124
Zaburi 124
Shukrani Kwa Ukombozi Wa Israeli
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.
1 #
Za 129:1; Mwa 15:1; Hes 14:9; Yos 1:5 Kama Bwana asingalikuwa upande wetu;
Israeli na aseme sasa:
2kama Bwana asingalikuwa upande wetu,
wakati watu walipotushambulia,
3 #
Za 35:25; Mit 1:12; Yer 51:34 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,
wangalitumeza tungali hai,
4 #
Za 88:17; 18:4 mafuriko yangalitugharikisha,
maji mengi yangalitufunika,
5maji yaendayo kasi
yangalituchukua.
6 Bwana asifiwe,
yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.
7 #
Za 91:3; 25:15 Tumeponyoka kama ndege
kutoka mtego wa mwindaji;
mtego umevunjika,
nasi tukaokoka.
8 #
1Sam 17:45; Mwa 1:1; Za 115:15; 121:2; 134:3; Kut 18:4; Mit 18:10; Isa 50:10 Msaada wetu ni katika jina la Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.