Zaburi 125
NEN

Zaburi 125

125
Zaburi 125
Usalama Wa Watu Wa Mungu
Wimbo wa kwenda juu.
1 # Za 46:5; 48:2-5; 48:12; Isa 33:20 Wale wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni,
ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.
2 # 1Nya 21:15; Za 32:10; Zek 2:4-5 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,
ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake
sasa na hata milele.
3 # Es 4:11; Za 89:22; Mit 22:8; Isa 13:11; 14:5; 24:10 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi
waliopewa wenye haki,
ili wenye haki wasije wakatumia
mikono yao kutenda ubaya.
4 # Za 119:65; 36:10 Ee Bwana, watendee mema walio wema,
wale walio wanyofu wa moyo.
5 # Ay 23:11; Isa 59:8; Za 92:7; 128:6; Mit 2:15; 17:6; Gal 6:16 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,
Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya.
Amani iwe juu ya Israeli.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014