Zaburi 126
NEN

Zaburi 126

126
Zaburi 126
Kurejezwa Kutoka Utumwani
Wimbo wa kwenda juu.
1 # Ezr 1:1-3; Za 85:1; Hos 6:11; Mdo 12:9 Bwana alipowarejeza mateka Sayuni,
tulikuwa kama watu walioota ndoto.
2 # Mwa 21:6; Ay 8:21; Kum 10:21; Za 65:8; 71:19; Lk 1:49 Vinywa vyetu vilijaa kicheko,
ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.
Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,
Bwana amewatendea mambo makuu.”
3 # Za 9:2; 16:11; 106:21; Yoe 2:21, 26 Bwana ametutendea mambo makuu,
nasi tumejaa furaha.
4 # Kum 30:3; Za 107:35; Isa 43:19; 51:3 Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa,
kama vijito katika Negebu.
5 # Za 16:11; 20:5; 23:6; 6:6; 80:5; Yer 50:4; Gal 6:9; Isa 12:1-3; 35:10; 51:11; 60:15; 61:7; Yer 31:6-7, 12 Wapandao kwa machozi
watavuna kwa nyimbo za shangwe.
6Yeye azichukuaye mbegu zake
kwenda kupanda, huku akilia,
atarudi kwa nyimbo za shangwe,
akichukua miganda ya mavuno yake.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014