127
Zaburi 127
Bila Mungu, Kazi Ya Mwanadamu Haifai
Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni.
1 #
Za 78:69; 121:4 Bwana asipoijenga nyumba,
wajengao hufanya kazi bure.
Bwana asipoulinda mji,
walinzi wakesha bure.
2 #
Mwa 3:17; Hes 6:26; Ay 11:18; Kum 33:12; Mhu 2:25 Mnajisumbua bure kuamka mapema
na kuchelewa kulala,
mkitaabikia chakula:
kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake.
3 #
Mwa 1:28; 33:5; Kum 28:4 Wana ni urithi utokao kwa Bwana,
watoto ni zawadi kutoka kwake.
4 #
Za 112:2
Kama mishale mikononi mwa shujaa
ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.
5 #
Za 128:2-3; Mwa 24:60; 23:10 Heri mtu ambaye podo lake
limejazwa nao.
Hawataaibishwa wanaposhindana
na adui zao langoni.