Zaburi 128
NEN

Zaburi 128

128
Zaburi 128
Thawabu Ya Kumtii Bwana
Wimbo wa kwenda juu.
1 # Za 103:11; 119:1-3 Heri ni wale wote wamchao Bwana,
waendao katika njia zake.
2 # Za 58:11; 109:11; Isa 3:10; Mwa 39:3; Mit 10:22 Utakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3 # Mwa 49:22; Ay 29:5; Mit 5:15; Eze 19:10; Za 52:8; 144:12 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
ndani ya nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4 # Za 1:1; 112:1 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Bwana.
5 # Za 122:9; 134:3 Bwana na akubariki kutoka Sayuni
siku zote za maisha yako,
na uone mafanikio ya Yerusalemu,
6 # Mwa 50:23; 48:11; Za 125:5 nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.
Amani iwe juu ya Israeli.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014