129
Zaburi 129
Maombi Dhidi Ya Adui Za Israeli
Wimbo wa kwenda juu.
1 #
Kut 1:13; Eze 23:3; Za 88:15; 124:1; Hos 2:15 Wamenionea mno tangu ujana wangu;
Israeli na aseme sasa:
2 #
Yer 1:19; 15:20; 20:11 wamenionea mno tangu ujana wangu,
lakini bado hawajanishinda.
3 #
Ebr 11:26
Wakulima wamelima mgongo wangu,
na kufanya mifereji yao mirefu.
4 #
Kut 9:27; 2The 1:6; Za 37:9; 140:5 Lakini Bwana ni mwenye haki;
amenifungua toka kamba za waovu.
5 #
Mik 4:11; Za 70:2 Wale wote waichukiao Sayuni
na warudishwe nyuma kwa aibu.
6 #
Isa 37:27; 2Fal 19:26; Za 102:11; 37:2; Yer 17:5-6 Wawe kama majani juu ya paa,
ambayo hunyauka kabla hayajakua;
7 #
Kum 28:38; Za 79:12 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,
wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8 #
Za 118:26; Rut 2:4 Wale wapitao karibu na wasiseme,
“Baraka ya Bwana iwe juu yako;
tunakubariki katika jina la Bwana.”