Zaburi 130
NEN

Zaburi 130

130
Zaburi 130
Kuomba Msaada
Wimbo wa kwenda juu.
1 # Ay 30:19 Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
2 # Za 27:7; 28:2, 6; 31:22; 86:6; 140:6; 2Nya 6:40 Ee Bwana, sikia sauti yangu.
Masikio yako na yawe masikivu
kwa kilio changu unihurumie.
3 # 1Sam 6:20; Ezr 9:15; Hes 1:6; Za 143:2; Ufu 6:17; Yn 8:7, 9; Rum 3:20 Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,
Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
4 # Kut 34:7; Efe 1:7; 2Sam 24:14; Yer 17:5-6; 31:34; 1Fal 8:40; 2The 1:6; Za 37:2; Ebr 12:28 Lakini kwako kuna msamaha,
kwa hiyo wewe unaogopwa.
5 # Isa 8:17; 26:8; 30:18; 49:23; Za 5:3; 119:74; 27:14 Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
6 # Za 63:6; 2Sam 23:4 Nafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
7 # 1Nya 21:13; Za 25:5; 71:14; 111:9; Rum 3:24; Isa 55:7 Ee Israeli, mtumaini Bwana,
maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
8 # Lk 1:68; Kut 34:7; Mt 1:21 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli
kutoka dhambi zao zote.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014