Zaburi 135
NEN

Zaburi 135

135
Zaburi 135
Wimbo Wa Sifa Kwa Mungu
1 # Neh 7:73 Msifuni Bwana.
Lisifuni jina la Bwana,
msifuni, enyi watumishi wa Bwana,
2 # 1Nya 15:2; Lk 2:37; Za 116:19 ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana,
katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.
3 # 1Nya 16:34; Za 119:68; 68:4; 92:1; 147:1 Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema,
liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.
4 # Kut 19:5; Kum 7:6, 7; 10:15; Mal 3:17; Tit 2:14 Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe,
Israeli kuwa mali yake ya thamani.
5 # Za 48:1; 145:3; Kut 12:12; 1Nya 16:25; Ay 21:22 Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu,
kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.
6 # Za 115:3; Dan 4:35; Mt 6:10 Bwana hufanya lolote apendalo,
mbinguni na duniani,
katika bahari na vilindi vyake vyote.
7 # Ay 5:10; Za 68:6; Isa 30:23; Amo 4:13; Yer 10:13; 51:16; Yoe 2:23; Zek 10:1; Kum 28:12; Mwa 2:6; Ay 28:25; 38:22 Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia;
hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua
na huleta upepo kutoka ghala zake.
8 # Kut 4:23; 12:12 Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,
mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.
9 # Kut 7:9; Za 136:10-15 Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri,
dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10 # Hes 21:21-25; Yos 24:8-11; Za 44:2; 78:55; 136:17-21 Aliyapiga mataifa mengi,
na akaua wafalme wenye nguvu:
11 # Hes 21:21, 26, 33; Yos 12:7-24 Mfalme Sihoni na Waamori,
Ogu mfalme wa Bashani
na wafalme wote wa Kanaani:
12 # Kum 29:8 akatoa nchi yao kuwa urithi,
urithi kwa watu wake Israeli.
13 # Kut 3:15; Za 102:12 Ee Bwana, jina lako ladumu milele,
kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote.
14 # 1Sam 24:15; Ebr 10:30; Kum 32:36 Maana Bwana atawathibitisha watu wake,
na kuwahurumia watumishi wake.
15 # Ufu 9:20; Isa 2:8; 31:7; 37:19; 40:19; Yer 1:16; 10:5; Za 96:5 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
16 # 1Fal 18:26 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
17 # Yer 10:14; Hab 2:19 zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.
18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
19 # Za 22:23 Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana;
ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;
20ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana;
ninyi mnaomcha, msifuni Bwana.
21 # Za 128:5; 134:3; 1Fal 8:13; 2Nya 6:2 Msifuni Bwana kutoka Sayuni,
msifuni yeye aishiye Yerusalemu.
Msifuni Bwana.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014