Zaburi 136
NEN

Zaburi 136

136
Zaburi 136
Wimbo Wa Kumshukuru Mungu
1 # Za 105:1; 100:5; 145:9; 118:1-4; 106:1; Ezr 3:11; Hes 2:26; 1:7; 2Nya 5:13; Yer 33:11 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema.
Fadhili zake zadumu milele.
2 # Za 105:1; Kum 10:17; Kut 18:11 Mshukuruni Mungu wa miungu.
Fadhili zake zadumu milele.
3 # Za 105:1; Kum 10:17; 1Tim 6:15 Mshukuruni Bwana wa mabwana:
Fadhili zake zadumu milele.
4 # Kut 3:20; Ay 9:10 Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu,
Fadhili zake zadumu milele.
5 # Mit 3:19; Yer 51:15; Mwa 1:1 Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu,
Fadhili zake zadumu milele.
6 # Mwa 1:1; 1:6; Isa 42:5; Yer 10:12; 33:2 Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji,
Fadhili zake zadumu milele.
7 # Mwa 1:14, 16; Za 74:16; Yak 1:17 Ambaye aliumba mianga mikubwa,
Fadhili zake zadumu milele.
8 # Mwa 1:16 Jua litawale mchana,
Fadhili zake zadumu milele.
9Mwezi na nyota vitawale usiku,
Fadhili zake zadumu milele.
10 # Kut 4:23; 12:12 Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,
Fadhili zake zadumu milele.
11 # Kut 6:6; 13:3; Za 105:43 Na kuwatoa Israeli katikati yao,
Fadhili zake zadumu milele.
12 # Kut 3:20; Kum 5:15; 9:29 Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa,
Fadhili zake zadumu milele.
13 # Za 78:13 Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu,
Fadhili zake zadumu milele.
14 # Kut 14:22; Za 106:9 Na kuwapitisha Israeli katikati yake,
Fadhili zake zadumu milele.
15 # Kut 14:27 Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu,
Fadhili zake zadumu milele.
16 # Kut 13:18; Za 78:52 Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa,
Fadhili zake zadumu milele.
17 # Hes 21:23-25; Yos 24:8-11; Za 78:55; 135:9-12 Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu,
Fadhili zake zadumu milele.
18 # Kum 29:7; Yos 12:7-24 Naye aliwaua wafalme wenye nguvu,
Fadhili zake zadumu milele.
19 # Hes 21:21-25 Sihoni mfalme wa Waamori,
Fadhili zake zadumu milele.
20 # Hes 21:33-35 Ogu mfalme wa Bashani,
Fadhili zake zadumu milele.
21 # Kum 1:38; Yos 12:1; 14:1 Akatoa nchi yao kuwa urithi,
Fadhili zake zadumu milele.
22 # Kum 29:8; Za 78:55; Isa 20:3; 41:8; 42:19; 43:10; 44:1, 21; 45:4; 49:5-7 Urithi kwa Israeli mtumishi wake,
Fadhili zake zadumu milele.
23 # Za 78:29; 103:14; 115:12 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu,
Fadhili zake zadumu milele.
24 # Yos 10:14; Neh 9:28; Kum 6:19 Alituweka huru toka adui zetu,
Fadhili zake zadumu milele.
25 # Mwa 1:30; Mit 6:26 Ambaye humpa chakula kila kiumbe.
Fadhili zake zadumu milele.
26 # Za 105:1; 115:3; Ezr 3:11 Mshukuruni Mungu wa mbinguni,
Fadhili zake zadumu milele.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014