139
Zaburi 139
Mungu Asiyeweza Kukwepwa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 17:3; 44:21; Rum 8:27 Ee Bwana, umenichunguza
na kunijua.
2 #
2Fal 19:27; Za 94:11; Mit 24:12; Yer 12:3 Unajua ninapoketi na ninapoinuka;
unatambua mawazo yangu tokea mbali.
3 #
2Fal 19:27; Ay 31:4 Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu;
unaelewa njia zangu zote.
4 #
Ebr 4:13
Kabla neno halijafika katika ulimi wangu,
wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.
5 #
1Sam 25:16; Za 32:10; 34:7; 125:2 Umenizunguka nyuma na mbele;
umeweka mkono wako juu yangu.
6 #
Za 131:1; Rum 11:33 Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu,
ni ya juu sana kwangu kuyafikia.
7 #
Yer 23:24
Niende wapi nijiepushe na Roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
8 #
Kum 30:12-15; Amo 9:2-3; Ay 17:13 Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko;
nikifanya vilindi#139:8 Vilindi ina maana ya Kuzimu, ambayo ni Sheol kwa Kiebrania. kuwa kitanda changu,
wewe uko huko.
9Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko,
kama nikikaa pande za mbali za bahari,
10 #
Za 23:3; 108:6; Isa 41:10 hata huko mkono wako utaniongoza,
mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.
11Kama nikisema, “Hakika giza litanificha
na nuru inayonizunguka iwe usiku,”
12 #
Ay 34:22; Dan 2:22 hata giza halitakuwa giza kwako,
usiku utangʼaa kama mchana,
kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.
13 #
Za 119:73; Ay 10:11; Isa 44:2, 24; 46:3; 49:5; Yer 1:5 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;
uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.
14Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa
kwa namna ya ajabu na ya kutisha;
kazi zako ni za ajabu,
ninajua hayo kikamilifu.
15 #
Mhu 11:5; Ay 10:11; Za 63:9 Umbile langu halikufichika kwako,
nilipoumbwa mahali pa siri.
Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,
16 #
Ay 33:29; Za 90:12 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.
Siku zangu zote ulizonipangia
ziliandikwa katika kitabu chako
kabla haijakuwepo hata moja.
17 #
Za 92:5; Ay 5:9 Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu!
Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!
18 #
Za 40:5; 3:5; Ay 29:18 Kama ningezihesabu,
zingekuwa nyingi kuliko mchanga.
Niamkapo,
bado niko pamoja nawe.
19 #
Za 5:6; 6:8; 59:2; Isa 11:4 Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu!
Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!
20 #
Za 65:7; Kum 5:11; Ay 21:14-15; Yud 15 Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya,
adui zako wanatumia vibaya jina lako.
21 #
2Nya 19:2; Za 31:6; 26:5; 119:113 Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia?
Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako?
22 #
Mt 5:43
Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao,
ninawahesabu ni adui zangu.
23 #
Ay 31:6; 1Sam 16:7; 1Nya 29:17; Za 7:9; Mit 17:3; Yer 11:20; Ufu 2:23 Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu,
nijaribu na ujue mawazo yangu.
24 #
Yer 25:5; 36:3; Za 5:8; 23:2; 143:10 Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu,
uniongoze katika njia ya milele.