Zaburi 14
NEN

Zaburi 14

14
Zaburi 14
Uovu Wa Wanadamu
(Zaburi 53)
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Za 10:4; Mwa 6:12; Rum 3:10; Mit 1:7, 22 Mpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa;
hakuna hata mmoja atendaye mema.
2 # Ay 41:34; Za 32:6; 85:11; 102:19; Ezr 6:21; Mao 3:50 Bwana anawachungulia wanadamu chini
kutoka mbinguni
aone kama wako wenye akili,
wowote wanaomtafuta Mungu.
3 # 1Sam 8:3; 2Pet 2:7; 1Tim 5:15; 1Fal 8:46; Za 143:2; Mhu 7:20; Rum 3:10-12 Wote wamepotoka,
wameharibika wote pamoja,
hakuna atendaye mema.
Naam, hakuna hata mmoja!
4 # Za 17:2; 82:5; 79:6; Mik 3:3; Isa 64:7; 65:1; Yer 4:22; 10:25; Hos 7:7 Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza:
wale ambao huwala watu wangu
kama watu walavyo mkate,
hao ambao hawamwiti Bwana?
5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,
maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.
6 # 2Sam 22:3 Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini,
bali Bwana ndiye kimbilio lao.
7 # Za 2:6; Yer 48:47; Kum 30:3 Laiti wokovu wa Israeli
ungalikuja kutoka Sayuni!
Wakati Bwana arejeshapo
wafungwa wa watu wake,
Yakobo na ashangilie,
Israeli na afurahi!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014