140
Zaburi 140
Kuomba Ulinzi Wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 17:13; 25:20; 59:2; 71:4; 142:6; 143:9; 86:14 Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu;
nilinde na watu wenye jeuri,
2 #
Mit 6:14; 16:27; Isa 59:4; Hos 7:15; Za 36:4; 52:2; 68:30 ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao,
na kuchochea vita siku zote.
3 #
Za 57:4; 58:4; Rum 3:13; Yak 3:8 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka,
sumu ya nyoka iko midomoni mwao.
4 #
Za 141:9; 36:11 Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu;
nilinde na watu wenye jeuri
wanaopanga kunikwaza miguu yangu.
5 #
Ay 34:30; Za 31:4; 38:12; 119:110; Ay 18:8; 18:9 Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa,
wametandaza kamba za wavu wao,
wametega mitego kwenye njia yangu.
6 #
Za 16:2; 28:2, 6 Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.”
Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.
7Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu,
unikingaye kichwa changu siku ya vita:
8 #
Za 10:2-3; 66:7; Ay 5:12-13 Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao,
usiache mipango yao ikafanikiwa,
wasije wakajisifu.
9 #
Mit 18:7
Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe
na shida zinazosababishwa na midomo yao.
10 #
Za 11:6; 21:9; Mt 3:10; Lk 12:40; Ufu 20:15 Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie!
Na watupwe motoni,
katika mashimo ya matope,
wasiinuke tena kamwe.
11 #
Za 34:21
Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi;
maafa na yawawinde watu wenye jeuri.
12 #
1Fal 8:45; Za 35:10; 82:3; 109:31 Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki,
na kuitegemeza njia ya mhitaji.
13 #
Za 138:2; 11:7; 16:11 Hakika wenye haki watalisifu jina lako,
na waadilifu wataishi mbele zako.