Zaburi 141
NEN

Zaburi 141

141
Zaburi 141
Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu
Zaburi ya Daudi.
1 # Za 22:19; 4:1; 5:1-2; 27:7; 143:1 Ee Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima.
Sikia sauti yangu ninapokuita.
2 # Lk 1:9; Ufu 5:8; 8:3; Za 28:2; 63:4; 1Tim 2:8; Kut 29:39, 41; 30:8; Efe 5:2 Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba;
kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.
3 # Za 34:13; 12:2; Yak 1:26; 3:8 Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu,
weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.
4 # Yos 24:23; Za 106:29; Mit 23:1-3 Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya,
nisije nikashiriki katika matendo maovu
pamoja na watu watendao mabaya,
wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.
5 # Mit 9:8; 19:25; 25:12; Mhu 7:5; Kut 29:7; Za 23:5 Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;
na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.
Kichwa changu hakitalikataa.
Hata hivyo, maombi yangu daima
ni kinyume cha watenda mabaya,
6 # 2Nya 25:12 watawala wao watatupwa chini
kutoka kwenye majabali,
waovu watajifunza kwamba maneno yangu
yalikuwa kweli.
7 # Za 129:3; Hes 16:32-33; 16:30; 2Kor 1:9 Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi,
ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.”
8 # Za 123:2; 2:12; 11:1 Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi,
ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.
9 # Za 140:4; 64:5; 38:12 Niepushe na mitego waliyonitegea,
kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya.
10 # Za 7:15; 35:8; 57:6; 124:7 Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,
wakati mimi ninapita salama.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014