Zaburi 142
NEN

Zaburi 142

142
Zaburi 142
Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Watesi
Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Maombi.
1 # 1Fal 8:52; Za 3:4; 30:8 Namlilia Bwana kwa sauti,
nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie.
2 # Za 64:1; 50:15 Namimina malalamiko yangu mbele zake,
mbele zake naeleza shida zangu.
3 # Za 6:2; 77:3; 84:2; 88:4; 143:4, 7; Yer 4:18; Mao 1:22 Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu,
wewe ndiwe unajua njia zangu.
Katika njia ninayopita
watu wameniwekea mtego.
4 # Yer 25:35; 30:17 Tazama kuume kwangu na uone,
hakuna hata mmoja anayejihusisha nami.
Sina kimbilio,
hakuna anayejali maisha yangu.
5 # Za 16:5; 27:13; 46:1; Kum 32:9; Ay 28:13; Mao 3:24 Ee Bwana, nakulilia wewe,
nasema, “Wewe ni kimbilio langu,
fungu langu katika nchi ya walio hai.”
6 # Za 17:1; 79:8; 25:20; Yer 31:11 Sikiliza kilio changu,
kwa sababu mimi ni mhitaji sana;
niokoe na wale wanaonifuatilia,
kwa kuwa wamenizidi nguvu.
7 # Za 66:11; 7:17; 9:2; 2Nya 6:41 Nifungue kutoka kifungo changu,
ili niweze kulisifu jina lako.
Ndipo wenye haki watanizunguka,
kwa sababu ya wema wako kwangu.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014