Zaburi 143
NEN

Zaburi 143

143
Zaburi 143
Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Adui
Zaburi ya Daudi.
1 # Za 141:1; 28:2; 130:2; 89:1-2 Ee Bwana, sikia sala yangu,
sikiliza kilio changu unihurumie;
katika uaminifu na haki yako
njoo unisaidie.
2 # Za 14:3; Rum 3:10; Ay 14:3; 4:17; Mhu 7:20; Gal 2:16 Usimhukumu mtumishi wako,
kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako.
3 # Za 107:10; 7:1, 2; Law 3:6 Adui hunifuatilia,
hunipondaponda chini;
hunifanya niishi gizani
kama wale waliokufa zamani.
4 # Za 30:7 Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu,
moyo wangu ndani yangu unakata tamaa.
5 # Za 77:6; 77:5, 11; Mwa 24:63 Nakumbuka siku za zamani;
natafakari juu ya kazi zako zote,
naangalia juu ya kazi
ambazo mikono yako imezifanya.
6 # Kut 9:29; Ay 11:13; Za 28:2 Nanyoosha mikono yangu kwako,
nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame.
7 # Za 69:17; 142:3; 22:24; 27:9; 30:7 Ee Bwana, unijibu haraka,
roho yangu inazimia.
Usinifiche uso wako,
ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni.
8 # Kut 33:13; Ay 34:32; Za 6:4; 90:14; 27:11; 32:8; 25:1-2; 86:4 Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma,
kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako.
Nionyeshe njia nitakayoiendea,
kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu.
9 # Za 140:1; 18:17; 31:15 Ee Bwana, uniokoe na adui zangu,
kwa kuwa nimejificha kwako.
10 # Za 119:12; 31:14; 25:4-5; 26:11; Neh 9:20; Yn 14:26; Rum 5:5; Efe 4:30; Gal 5:22, 23 Nifundishe kufanya mapenzi yako,
kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu,
Roho wako mwema na aniongoze
katika nchi tambarare.
11 # Za 25:11; 41:2; 31:1; 71:2 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu,
kwa haki yako nitoe katika taabu.
12 # Za 8:2; 54:5; 116:16 Kwa upendo wako usiokoma,
nyamazisha adui zangu;
waangamize watesi wangu wote,
kwa kuwa mimi ni mtumishi wako.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014