144
Zaburi 144
Mfalme Amshukuru Mungu Kwa Ushindi
Zaburi ya Daudi.
1 #
Mwa 49:24; 2Sam 22:35 Sifa ni kwa Bwana Mwamba wangu,
aifundishaye mikono yangu vita,
na vidole vyangu kupigana.
2 #
Za 59:9; 91:2; 18:39; 27:1; 37:39; 43:2; 18:2; Amu 4:23; Mwa 15:1 Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu,
ngome yangu na mwokozi wangu,
ngao yangu ninayemkimbilia,
ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.
3 #
Ebr 2:6
Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali,
Binadamu ni nini hata umfikirie?
4 #
Ay 7:7; 27:3; 14:2; Isa 2:22; 1Nya 29:15; Yak 4:14 Mwanadamu ni kama pumzi,
siku zake ni kama kivuli kinachopita.
5 #
Za 18:9; 57:3; 104:32; Isa 64:1; Mwa 11:5 Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke,
gusa milima ili itoe moshi.
6 #
Hab 3:11; Zek 9:14; Za 59:11; 68:1; 7:12, 13; 18:14 Peleka umeme uwatawanye adui,
lenga mishale yako uwashinde.
7 #
2Sam 22:17; Za 3:7; 57:3; 69:2; 18:44 Nyoosha mkono wako kutoka juu,
nikomboe na kuniokoa
kutoka maji makuu,
kutoka mikononi mwa wageni
8 #
Za 12:2; 41:6; 26:3; Mwa 14:22; Kum 32:40 ambao vinywa vyao vimejaa uongo,
na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.
9 #
Za 28:7; 96:1; 33:2-3; 71:22; 69:1 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,
kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,
10 #
2Sam 8:14; Za 18:50; Ay 5:20 kwa Yule awapaye wafalme ushindi,
ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari.
11 #
Za 3:7; 25:20; 18:44; 41:6-7; 12:2; 36:3; 106:26; Isa 44:20 Nikomboe na uniokoe
kutoka mikononi mwa wageni
ambao vinywa vyao vimejaa uongo,
na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.
12 #
Za 92:12-14; 128:3; 4:4; 7:4 Kisha wana wetu wakati wa ujana wao
watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri,
binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa
kurembesha jumba la kifalme.
13 #
Mit 3:10
Ghala zetu zitajazwa
aina zote za mahitaji.
Kondoo zetu watazaa kwa maelfu,
kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu;
14 #
Mit 14:4; 2Fal 25:11; Isa 24:11; Yer 14:2-3; Law 26:17 maksai wetu watakokota
mizigo mizito.
Hakutakuwa na kubomoka kuta,
hakuna kuchukuliwa mateka,
wala kilio cha taabu
katika barabara zetu.
15 #
Kum 28:3; 33:29 Heri watu ambao hili ni kweli;
heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.