Zaburi 146
NEN

Zaburi 146

146
Zaburi 146
Kumsifu Mungu Mwokozi
1 # Za 103:1; 104:1 Msifuni Bwana!#146:1 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.
Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,
2 # Za 104:33; 63:4; 105:2 Nitamsifu Bwana maisha yangu yote;
nitamwimbia Mungu wangu sifa
wakati wote niishipo.
3 # Za 118:9; 60:11; 108:12; Isa 2:22 Usiweke tumaini lako kwa wakuu,
kwa wanadamu ambao hufa,
ambao hawawezi kuokoa.
4 # Mhu 12:7; Mwa 3:19; Ay 7:21; 1Kor 2:6; Za 103:14; 33:10 Roho yao itokapo hurudi mavumbini,
siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.
5 # Za 119:43; 37:9; 144:15; 33:18; 71:5; 70:5; 121:2; Yer 17:7 Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,
6 # 2Nya 2:12; Za 18:25; 108:4; 117:2; 115:15; Mdo 14:15; Kum 7:9; Mik 7:20; Ufu 10:6; 14:7 Muumba wa mbingu na nchi,
na bahari na vyote vilivyomo ndani yake:
Bwana anayedumu kuwa mwaminifu
milele na milele.
7 # Za 37:17; 103:6; 107:9; 145:15; 66:11; 68:6 Naye huwapatia haki walioonewa
na kuwapa wenye njaa chakula.
Bwana huwaweka wafungwa huru,
8 # Isa 32:3; 29:18; 35:5; 42:7, 18, 19; 43:8; Ay 23:10; Kut 4:11; Za 38:6; Kum 7:13; Mt 11:5; Mit 20:12 Bwana huwafumbua vipofu macho,
Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao,
Bwana huwapenda wenye haki.
9 # Law 19:34; Za 10:18; Kut 22:22; Yak 1:27 Bwana huwalinda wageni
na kuwategemeza yatima na wajane,
lakini hupinga njia za waovu.
10 # Mwa 21:33; 1Nya 16:31; Za 93:1; 99:1; Ufu 11:15 Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, ee Sayuni,
kwa vizazi vyote.
Msifuni Bwana.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014