147
Zaburi 147
Kumsifu Mungu Mwenye Nguvu Zote
1 #
Za 135:3; 33:1 Msifuni Bwana.
Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa,
jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!
2 #
Za 51:18; 106:47; Kum 30:3; Isa 27:13; Yer 32:37; Eze 36:24 Bwana hujenga Yerusalemu,
huwakusanya Israeli walio uhamishoni.
3 #
Za 34:18; Isa 1:6; 61:1; Eze 34:16; Ebr 12:13; Ay 5:18; Lk 4:18 Anawaponya waliovunjika mioyo
na kuvifunga vidonda vyao.
4 #
Mwa 15:5; Isa 40:26 Huzihesabu nyota
na huipa kila moja jina lake.
5 #
Kut 14:31; Nah 1:3; 1Nya 16:25; Za 48:1; 145:3; Isa 40:28 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,
ufahamu wake hauna kikomo.
6 #
2Nya 33:23; Za 146:8, 9; 37:9, 10; 145:20 Bwana huwahifadhi wanyenyekevu
lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.
7 #
Za 30:4; 33:3; 42:4; 27:6; 98:5; Efe 2:20 Mwimbieni Bwana kwa shukrani,
mpigieni Mungu wetu kinubi.
8 #
Kum 32:2; 11:14; 2Sam 1:21; Ay 26:8; 38:26; 5:10; 28:26; Za 104:14 Yeye huzifunika anga kwa mawingu,
huinyeshea ardhi mvua,
na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.
9 #
Ay 38:41; Mt 6:26; Mwa 8:7; 1:30; Lk 12:24; Za 104:27, 28 Huwapa chakula mifugo
na pia makinda ya kunguru yanapolia.
10 #
1Sam 16:7; Hos 1:7; Ay 39:11; Za 33:16-17 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi,
wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.
11 #
Za 35:27; 33:18; 103:11; 119:43; 6:4 Bwana hupendezwa na wale wamchao,
wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.
12 #
Za 48:1
Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu,
msifu Mungu wako, ee Sayuni,
13 #
Kum 33:25; Law 25:21; Za 128:5; 134:3 kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako
na huwabariki watu wako walio ndani yako.
14 #
Law 26:6; 2Sam 7:10; Isa 48:18; Za 132:15; Kum 32:14 Huwapa amani mipakani mwenu
na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.
15 #
Ay 37:12; Za 33:9; 148:5; Isa 55:11 Hutuma amri yake duniani,
neno lake hukimbia kasi.
16 #
Za 148:8; Ay 37:12; 38:29 Anatandaza theluji kama sufu
na kutawanya umande kama majivu.
17 #
Kut 9:22, 23; Ay 38:22; Za 78:47 Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe.
Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?
18 #
Za 33:9; 107:20; 50:3 Hutuma neno lake na kuviyeyusha,
huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.
19 #
Kut 20:1; Mal 4:4; Za 78:5; Yos 1:8; Kum 33:4; 2Fal 22:8; Rum 3:2; 9:4 Amemfunulia Yakobo neno lake,
sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.
20 #
Rum 3:1-2; Kum 4:7-8, 32-34; Za 79:6; 103:1; 33:2; Mdo 14:16 Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote,
hawazijui sheria zake.
Msifuni Bwana.