Zaburi 148
NEN

Zaburi 148

148
Zaburi 148
Mwito Kwa Ulimwengu Kumsifu Mungu
1 # Za 33:2; 103; 1; 19:1; 69:34; 150:1 Msifuni Bwana.
Msifuni Bwana kutoka mbinguni,
msifuni juu vileleni.
2 # Za 103:20; 1Fal 22:19; Dan 7:10; Ebr 1:7 Msifuni, enyi malaika wake wote,
msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.
3 # Za 19:1 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi,
msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.
4 # Kum 10:14; Mwa 1:7; 1Fal 8:27 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana,
na ninyi maji juu ya anga.
5 # Za 145:21; 147:15; Ebr 11:3 Vilisifu jina la Bwana
kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.
6 # Yer 31:35-36; 33:25; 33:25 Aliviweka mahali pake milele na milele,
alitoa amri ambayo haibadiliki milele.
7 # Za 33:2; 74:13, 14; Mwa 1:21; Isa 43:20; Kum 33:13 Mtukuzeni Bwana kutoka duniani,
ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,
8 # Yos 10:11; Ay 37:11, 12; Za 147:15-18; 103:20; Kut 9:18 umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu,
pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,
9 # Isa 44:23; 49:13; 55:12 ninyi milima na vilima vyote,
miti ya matunda na mierezi yote,
10 # Isa 43:20; Hos 2:18 wanyama wa mwituni na mifugo yote,
viumbe vidogo na ndege warukao,
11 # Za 102:15; Mdo 17:28 wafalme wa dunia na mataifa yote,
ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,
12wanaume vijana na wanawali,
wazee na watoto.
13 # Za 113:2; 138:4; 145:5; 8:1; Isa 6:3; Flp 2:9 Wote na walisifu jina la Bwana,
kwa maana jina lake pekee limetukuka,
utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.
14 # Kut 15:2; 1Pet 2:9; Za 22:3; 145:10; Kum 26:19; Efe 2:17; 1Sam 1:2 Amewainulia watu wake pembe,#148:14 Pembe hapa inawakilisha mwenye nguvu, yaani mfalme.
sifa ya watakatifu wake wote,
ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake.
Msifuni Bwana.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014