Zaburi 149
NEN

Zaburi 149

149
Zaburi 149
Wimbo Wa Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake
1 # Za 33:2; 103:1; 28:7; 1:5; 96:1; Ufu 5:9; Isa 42:10 Msifuni Bwana.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.
2 # Yer 51:48; Zek 9:9; Za 10:16; 47:6; 95:6; Ay 35:10; 10:3; Isa 13:3; 32:1; 44:2; 45:11; 54:5 Israeli na washangilie katika Muumba wao,
watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.
3 # Kut 15:20; Za 57:8 Na walisifu jina lake kwa kucheza
na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
4 # Za 35:27; 147:11; 132:16; Mit 11:20 Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake,
anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.
5 # Za 132:16; 42:8; Ay 35:10 Watakatifu washangilie katika heshima hii,
na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.
6 # Za 66:17; Ebr 4:12; Ufu 1:16; Neh 4:17; Kum 7:1, 2 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao
na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
7 # Hes 31:3; Kum 32:41; Za 81:15 ili walipize mataifa kisasi
na adhabu juu ya mataifa,
8 # 2Sam 3:34; Isa 14:1-2; 2Nya 33:11 wawafunge wafalme wao kwa minyororo,
wakuu wao kwa pingu za chuma,
9 # Kum 7:1; 1Yn 5:4; Eze 28:26; Za 145:10; Rum 16:20 ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao.
Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote.
Msifuni Bwana.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014