15
Zaburi 15
Kitu Mungu Anachotaka
Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 27:4; 23:6; 2:5; 61:4; 20:2; 78:69; 150:1; Kut 29:46; 25:8; 15:17; 1Nya 22:19 Bwana, ni nani awezaye kukaa
katika Hekalu lako?
Nani awezaye kuishi
katika mlima wako mtakatifu?
2 #
1The 3:13; Tit 1:6; Mit 16:13; Rum 9:1; Isa 38:15, 16; 45:19; Yer 7:28; 9:5; Mwa 6:9; Efe 1:4; 4:25; Za 18:32; 84:11; Zek 8:3, 16 Ni yule aendaye pasipo mawaa,
atendaye yaliyo haki,
asemaye kweli toka moyoni mwake,
3 #
Law 19:16
na hana masingizio ulimini mwake,
asiyemtenda jirani yake vibaya,
na asiyemsingizia mwenzake,
4 #
Ay 19:9; Yos 9:18; Mdo 28:10; Kum 23:21; Mt 5:33 ambaye humdharau mtu mbaya,
lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana,
yule atunzaye kiapo chake
hata kama anaumia.
5 #
Kut 22:25; 18:21; Mdo 24:26; 2Pet 1:10; Za 21:7; 112:6; Ay 29:18; Ebr 12:28 Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,
na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.
Mtu afanyaye haya
kamwe hatatikisika.