150
Zaburi 150
Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake
1 #
Za 112:1; 73:17; 68:24-26; 102:19; 148:1 Msifuni Bwana.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake,
msifuni katika mbingu zake kuu.
2 #
Kum 3:24; Kut 15:7 Msifuni kwa matendo yake makuu,
msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 #
Hes 10:2; Za 57:8 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,
msifuni kwa kinubi na zeze,
4 #
Kut 15:20; Za 45:8; Isa 38:20; Mwa 4:21 msifuni kwa matari na kucheza,
msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
5 #
2Sam 6:5
msifuni kwa matoazi yaliayo,
msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 #
Za 103:22; Ufu 5:13 Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.
Msifuni Bwana!