16
Zaburi 16
Sala Ya Matumaini
Utenzi wa Daudi.
1 #
Za 25:20; 12:7; 2:12 Ee Mungu, uniweke salama,
kwa maana kwako nimekimbilia.
2 #
Za 31:14; 73:25; 118:28; 140:6 Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu;
pasipo wewe sina jambo jema.”
3 #
Kum 33:3; Rum 1:7; Dan 7:18; Mdo 9:13; Za 30:4; 85:8; 101:6 Kwa habari ya watakatifu walioko duniani,
ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.
4 #
Za 32:10; Kut 13:13; 18:11; 20:3; Mit 23:29; Kum 18:19; 31:20 Huzuni itaongezeka kwa wale
wanaokimbilia miungu mingine.
Sitazimimina sadaka zao za damu
au kutaja majina yao midomoni mwangu.
5 #
Law 2:2; Za 23:5; 75:8; 116:13; Isa 51:17; Hab 2:16; Ay 22:26; Mao 4:21 Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu;
umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.
6 #
Kum 19:14; Za 104:9; Ay 22:26; Mit 8:29; Yer 5:22 Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri,
hakika nimepata urithi mzuri.
7 #
Za 73:24; 42:8; 77:6; Mit 15:22; Isa 11:2; Ay 35:10 Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri,
hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.
8 #
Isa 36:15; 37:20 #
1Fal 2:19; 1Nya 6:39; Za 73:23; 15:5 Nimemweka Bwana mbele yangu daima.
Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,
sitatikisika.
9 #
Za 4:7; 13:5; 28:7; 30:11; Kum 33:26 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia;
mwili wangu nao utapumzika salama,
10 #
Za 30:3; 31:17; 49:15; 86:13; Mdo 2:27, 31; 13:35; Hos 13:14; 2Fal 19:22; Lk 1:35; Ay 17:14; Dan 9:24; Hes 16:30 kwa maana hutaniacha kaburini,
wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.
11 #
Mdo 2:25-28; Mt 7:14; Isa 29:13; Za 139:24; 21:6; 80:1, 17; 30:10; 64:1; 140:6; 5:1, 2; 39:12; 142:6 Umenijulisha njia ya uzima;
utanijaza na furaha mbele zako,
pamoja na furaha za milele
katika mkono wako wa kuume.