18
Zaburi 18
Wimbo Wa Daudi Wa Ushindi
(2 Samweli 22:1-51)
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana aliyomwimbia Bwana wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Alisema hivi:
1 #
Kut 15:2; Yer 16:19; Kum 32:4; 33:29; Za 91:2; 22:19; 59:9; 81:1; 1Sam 2:2; Isa 2:10; 12:2; 49:5 Nakupenda wewe, Ee Bwana,
nguvu yangu.
2 #
Kut 33:22; Isa 2:1; 17:10; Yer 16:19; Za 40:17; 114:2; 2:12; 9:9; 94:20; 28:7, 8; 31:2, 3; 84:9; 119:114; Ebr 2:13; Mwa 15:1; Lk 1:69 Bwana ni mwamba wangu,
ngome yangu na mwokozi wangu,
Mungu wangu ni mwamba,
ambaye kwake ninakimbilia.
Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu,
ngome yangu.
3 #
1Nya 16:25; Za 9:13; 76:4 Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa,
nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
4 #
Za 116:4; 93:4; 124:6; Eze 43:2; Isa 5:30; 17:12; Yer 6:23; 51:42, 55 Kamba za mauti zilinizunguka,
mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
5 #
Mit 14:13
Kamba za kuzimu zilinizunguka,
mitego ya mauti ilinikabili.
6 #
Kum 4:30; Za 30:2; 99:6; 102; 120:1; 66:19; 116:1; Ay 16:18 Katika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu anisaidie.
Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika mbele zake,
masikioni mwake.
7 #
Za 97:4; Isa 5:25; 64:3; Amu 5:4, 5; Ay 9:5; Yer 10:10; Mdo 4:31 Dunia ilitetemeka na kutikisika,
misingi ya milima ikatikisika,
vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.
8 #
Ay 41:20, 21; Kut 15:17; 19:18; Mit 25:22; Za 50:3; 97:3; Dan 7:10; Rum 12:20 Moshi ukapanda kutoka puani mwake,
moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yawakayo
yakatoka ndani mwake.
9 #
Mwa 11:5; Isa 64:1; Za 57:3; 104:3; Kut 20:21; Kum 33:26 Akazipasua mbingu akashuka chini,
mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
10 #
Mwa 3:24; Eze 10:18; Kum 33:26; Za 104:3; 99:1 Alipanda juu ya kerubi akaruka,
akapaa juu kwa mbawa za upepo.
11 #
Za 97:2; Kut 19:9; Ay 22:14; Isa 4:5; Kum 4:11; Yer 43:10 Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika,
hema lake kumzunguka,
mawingu meusi ya mvua ya angani.
12 #
Za 104:2; Yos 10:10; Ay 36:30 Kutokana na mwanga wa uwepo wake
mawingu yalisogea,
ikanyesha mvua ya mawe
na umeme wa radi.
13 #
Kut 9:23; Za 29:3; 2Sam 2:10 Bwana alinguruma kutoka mbinguni,
sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
14 #
Kum 32:23; Ay 6:4; 36:30; Ufu 4:5; Za 21:12; Amu 4:15; Hes 24:8 Aliipiga mishale yake na kutawanya adui,
naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.
15 #
Za 11:3; 76:6; 104:7; 106:9; Isa 50:2; Kut 15:8 Mabonde ya bahari yalifunuliwa,
na misingi ya dunia ikawa wazi
kwa kukaripia kwako, Ee Bwana,
kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.
16 #
Kut 15:5; Mit 18:4; 20:5; Za 69:2; 144:7 Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;
alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
17 #
Za 38:19; 59:1; 143:9; Amu 18:26 Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,
kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
18 #
Mit 1:27; 16:4; Yer 17:17; 40:2; Oba 1:13; Za 20:2; Isa 3:1 Walinikabili siku ya msiba wangu,
lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
19 #
Za 31:8; 118:5; Hes 14:8 Alinileta nje mahali penye nafasi tele,
akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
20 #
1Sam 22:21; 26:23; Ay 22:30; Za 24:4; Rum 2:12; 2Nya 15:7; 1Kor 3:8; Mit 6:4 Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
21 #
2Nya 34:33; Za 37:34; 119:2; 102; Mit 8:32; 23:26 Kwa maana nimezishika njia za Bwana;
sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
22 #
Za 119:30
Sheria zake zote zi mbele yangu,
wala sijayaacha maagizo yake.
23 #
Mwa 6:9
Nimekuwa sina hatia mbele zake,
nami nimejilinda nisitende dhambi.
24 #
1Sam 26:23; Rut 2:12; Mt 10:41-42 Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.
25 #
Za 31:23; 37:23; 50:5; 25:10; 40:11; 89:24; 146:6; Mit 2:8; Mt 18:32-35 Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu,
kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia.
26 #
Mit 15:26; Mt 5:8; Flp 1:10; 1Tim 5:22; Tit 1:15; 1Yn 3:3; Mit 3:34; Mt 10:16; Lk 16:8; Law 26:23 Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu,
lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi.
27 #
2Nya 33:23; Mt 23:12; Ay 41:34; Za 10:5; Mit 3:33-35; 6:17 Wewe huwaokoa wanyenyekevu,
lakini huwashusha wenye kiburi.
28 #
1Fal 11:36; Za 132:17; Ay 29:3; Za 97:11; 112:4; Yn 1:5; Mdo 26:18; 2Kor 4:6; 2Pet 1:19; Ay 18:6 Wewe, Ee Bwana, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka;
Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga.
29 #
Isa 45:5; Ebr 11:34 Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi,
nikiwa pamoja na Mungu wangu
nitaweza kuruka ukuta.
30 #
Kum 32:4; Za 12:6; 3:3; 2:12; Mit 30:5; Ufu 15:3; Rum 12:3 Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu,
neno la Bwana halina dosari.
Yeye ni ngao kwa wote
wanaokimbilia kwake.
31 #
Kum 4:5; 32:39; Za 35:10; 86:8; 89:6; Isa 46:9; 44:6, 8; 45:5, 6, 14, 18, 21; Mwa 49:24 Kwa maana ni nani aliye Mungu
zaidi ya Bwana?
Ni nani aliye Mwamba
isipokuwa Mungu wetu?
32 #
1Pet 5:10; Yak 3:2; Za 15:2; 19:13; Ebr 10:14 Mungu ndiye anivikaye nguvu
na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
33 #
Za 42:1; Mit 5:19; Isa 35:6; Hab 3:19; Kum 32:13 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu,
huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
34 #
Za 144:1
Huifundisha mikono yangu kupigana vita;
mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
35 #
Za 3:5; 37:5, 17; 41:3; 51:2; 54:4; 55:22; 119:116; Isa 41:4, 10, 13; 43:2; 46:4 Hunipa ngao yako ya ushindi,
nao mkono wako wa kuume hunitegemeza,
unajishusha chini ili kuniinua.
36 #
Ay 18:7; Za 31:8; 66:9 Huyapanua mapito yangu,
ili miguu yangu isiteleze.
37 #
Law 26:7
Niliwafuatia adui zangu na nikawapata,
sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
38 #
Za 68:21; 110:6; 36:12; 47:3; 140:10; Isa 26:14 Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena;
walianguka chini ya miguu yangu.
39 #
Za 18:32, 47; Isa 45:5, 24; Za 47:3; 144:2 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;
uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
40 #
Yos 7:12; Za 18:37 Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,
nami nikawaangamiza adui zangu.
41 #
2Fal 14:26; Za 50:22; 1Sam 8:18; 14:37; Yer 11:11; Mit 1:28 Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa;
walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.
42 #
Kum 9:21; Isa 2:22 Niliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo;
niliwamwaga nje kama tope barabarani.
43 #
2Sam 8:1-14; Isa 55:5 Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu;
umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa,
watu ambao sikuwajua wananitumikia.
44 #
Za 144:7, 11; 54:3; Isa 25:5 Mara wanisikiapo hunitii,
wageni hunyenyekea mbele yangu.
45 #
2Kor 4:1; Ebr 12:3; 1Sam 17:32; Isa 66:2; Hos 3:5; 11:10; Za 9:9; Mik 7:17 Wote wanalegea,
wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.
46 #
Yos 3:10; 2Kor 13:4; 1Sam 14:39; Kut 33:22; Za 21:13; 35:27; 40:16; 108:5; 1Nya 16:35; Lk 1:47; Yer 10:10 Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!
Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!
47 #
Mwa 4:24; Za 18:29; Amu 4:23 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,
awatiishaye mataifa chini yangu,
48 #
Dan 3:17; Za 7:10; 37:40; 140:2; 18:49 aniokoaye na adui zangu.
Uliniinua juu ya adui zangu;
uliniokoa toka kwa watu wajeuri.
49 #
Za 101:1; 7:17; 9:2; 108:1; 146:2; Rum 15:9 Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana;
nitaliimbia sifa jina lako.
50 #
2Sam 23:1; Za 144:10; 89:4 Humpa mfalme wake ushindi mkuu,
huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake,
kwa Daudi na wazao wake milele.