Zaburi 2
NEN

Zaburi 2

2
Zaburi 2
Mfalme Aliyechaguliwa Na Mungu
1 # Za 21:11; 83:5; Mit 24:2 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,
na kabila za watu kula njama bure?
2 # Za 45:7; 48:4; 1Sam 9:16; Yn 1:41; Mdo 4:25-26 # Mao 3:55; Za 22:2; 55:17; 142:5; 42:7 Wafalme wa dunia wanajipanga
na watawala wanajikusanya pamoja
dhidi ya Bwana
na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
3 # Ay 36:8; Lk 19:14; 2Sam 3:34 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao
na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
4 # Za 11:4; Isa 37:16; 40:22; 66:1; Za 37:13; Mit 1:26 Yeye atawalaye mbinguni hucheka,
Bwana huwadharau.
5 # Za 6:1; 27:9; 38:1; 21:9; 79:6; 90:7; 110:5 Kisha huwakemea katika hasira yake
na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
6 # Za 10:16; 24:10; 9:11; 48:2, 11; 78:6; 110:2; 133:3; 2Fal 19:31; Kut 15:17 “Nimemtawaza Mfalme wangu
juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
Ushindi Wa Mfalme
7 # Mt 3:17; 8:29; 2Sam 7:14; Ebr 1:5; 5:5; Mdo 13:33 Nitatangaza amri ya Bwana:
Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu,
leo mimi nimekuzaa.
8 # Ay 22:26; Za 22:27; 67:7; Dan 7:13, 14; Mt 21:38 Niombe, nami nitayafanya mataifa
kuwa urithi wako,
miisho ya dunia kuwa milki yako.
9 # Mwa 49:10; Ufu 2:27; 12:5; 19:15; Mt 21:44; Kut 15:6; Isa 30:14; Yer 19:10 Utawatawala kwa fimbo ya chuma
na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”
10 # Za 141:6; Amu 2:3; Mit 8:15; 27:11 Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima;
mwonyeke, enyi watawala wa dunia.
11 # 1Nya 16:30; Za 9:2; 35:9; Isa 61:10 Mtumikieni Bwana kwa hofu
na mshangilie kwa kutetemeka.
12 # Kum 9:8; Za 5:11; 34:8; 64:10; Yer 17:7; Ufu 6:16; Yn 5:22, 23 Mbusu Mwana, asije akakasirika
nawe ukaangamizwa katika njia yako,
kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.
Heri wote wanaomkimbilia.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014