21
Zaburi 21
Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
1Sam 2:10; 2Sam 22:51 Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako.
Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake
kwa ushindi unaompa!
2 #
Za 20:4; Yn 11:42 Umempa haja ya moyo wake
na hukumzuilia maombi ya midomo yake.
3 #
2Sam 12:30; Ufu 14:14; Zek 6:11 Ulimkaribisha kwa baraka tele
na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
4 #
Za 10:16; 45:17; 48:14; 133:3; 2Sam 7:19 Alikuomba maisha, nawe ukampa,
wingi wa siku milele na milele.
5 #
Za 18:50; 44:4; 8:5; 45:3; 93:1; 96:6; 104:1 Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa,
umeweka juu yake fahari na utukufu.
6 #
Za 43:4; 126:3; 1Nya 17:27 Hakika umempa baraka za milele,
umemfanya awe na furaha
kwa shangwe ya uwepo wako.
7 #
2Fal 18:5; Za 6:4; 15:5; 55:22; 91:7; Mwa 14:18 Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana;
kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.
8 #
Isa 10:10
Mkono wako utawashika adui zako wote,
mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.
9 #
Kum 32:22; Yer 15:14 Wakati utakapojitokeza
utawafanya kama tanuru ya moto.
Katika ghadhabu yake Bwana atawameza,
moto wake utawateketeza.
10 #
Kum 28:18
Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani,
uzao wao kutoka wanadamu.
11 #
Za 2:1; 10:2; 26:10; 37:7; Ay 10:3 Ingawa watapanga mabaya dhidi yako
na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,
12 #
Kut 23:27
kwa kuwa utawafanya wakimbie
utakapowalenga usoni pao
kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.
13 #
Za 18:46; Ufu 15:3, 4 Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako,
tutaimba na kusifu nguvu zako.