22
Zaburi 22
Kilio Cha Uchungu Na Wimbo Wa Sifa
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 9:10; 10:1; Mt 27:46; Ay 3:24; 6:15; Mk 15:34; Ebr 5:7 Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa?
Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?
2 #
Ay 19:7; Za 42:3; 88:1 Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu,
hata usiku, sinyamazi.
3 #
2Fal 19:22; Za 71:22; 148:14; Mk 1:24; Ufu 4:8; Kut 15:2; Isa 6:3 Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu;
wewe ni sifa ya Israeli.#22:3 Tafsiri zingine zinasema: uketiye juu ya sifa za Israeli.
4 #
Za 78:53; 107:6 Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao,
walikutumaini nawe ukawaokoa.
5 #
1Nya 5:20; Rum 9:33; Za 25:3; 31:17; 71:1; 2Nya 13:18; Isa 8:17; 25:9; 26:3; 30:18; 49:23 Walikulilia wewe na ukawaokoa,
walikutegemea wewe nao hawakuaibika.
6 #
Ay 4:19; Mt 16:21; Mal 2:9; Isa 60:14; 49:7; 53:3; Za 119:141; 64:8; 109:25; 69:19; 2Sam 12:14 Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu,
wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.
7 #
Mt 9:24; 27:41; Mk 15:20, 29, 31, 32; Lk 16:14; 23:36, 39; Mt 27:39, 44; Ay 17:2; Za 35:16; 69:12; 74:18 Wote wanionao hunidhihaki,
hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao:
8 #
Za 91:14; 3:2; 2Sam 22:20; Mt 3:17; 27:43 Husema, “Anamtegemea Bwana,
basi Bwana na amwokoe.
Amkomboe basi, kwa maana
anapendezwa naye.”
9 #
Ay 10:18; Hes 1:7; Za 71:6; 78:7 Hata hivyo ulinitoa tumboni,
ukanifanya nikutegemee,
hata nilipokuwa ninanyonya
matiti ya mama yangu.
10 #
Za 71:6; Isa 46:3; 49:1 Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa,
toka tumboni mwa mama yangu
umekuwa Mungu wangu.
11 #
Za 10:1, 14; 2Fal 14:26; Isa 41:28 Usiwe mbali nami,
kwa maana shida iko karibu
na hakuna wa kunisaidia.
12 #
Za 69:30; 17:9; 27:6; 49:5; 109:3; 140:9; Kum 32:14; Isa 2:3; Eze 27:6; 39:18; Amo 4:1 Mafahali wengi wamenizunguka,
mafahali wa Bashani wenye nguvu
wamenizingira.
13 #
Eze 22:25; Sef 3:3; Mwa 49:9; 1Pet 5:8; Mao 3:6; Za 35:21 Simba wangurumao wanaorarua mawindo
yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.
14 #
Za 6:2
Nimemiminwa kama maji,
mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake.
Moyo wangu umegeuka kuwa nta,
umeyeyuka ndani yangu.
15 #
Isa 45:9; Yn 19:28; Za 137:6; 104:29; Mao 4:4; Ay 7:21; Eze 3:26 Nguvu zangu zimekauka kama kigae,
ulimi wangu umegandamana
na kaakaa la kinywa changu,
kwa sababu umenilaza
katika mavumbi ya kifo.
16 #
Flp 3:2; Isa 51:9; 53:5; Mit 17:22; Zek 12:10; Yn 20:25 Mbwa wamenizunguka,
kundi la watu waovu limenizingira,
wametoboa mikono yangu na miguu yangu.
17 #
Lk 23:35; Mik 7:8; Za 25:2; 30:1; 35:19; 38:16; Mao 2:17 Naweza kuhesabu mifupa yangu yote,
watu wananikodolea macho na kunisimanga.
18 #
Law 16:8; Yn 19:24; Mt 27:35; Mk 9:12; 15:24; Lk 23:34 Wanagawana nguo zangu wao kwa wao,
na vazi langu wanalipigia kura.
19 #
Za 18:1; 38:22; 70:5; 14:1; 40:13 Lakini wewe, Ee Bwana,
usiwe mbali.
Ee Nguvu yangu,
uje haraka unisaidie.
20 #
Ay 5:20; Za 141:1; 40:13 Okoa maisha yangu na upanga,
uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.
21 #
Ay 4:10, 12; Ebr 2:12; Hes 23:22; Za 22:13; 68:26; 40:9, 10; 35:18; 2Tim 4:17 Niokoe kutoka kinywani mwa simba,
niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.
22 #
Za 26:12; 35:18; 40:9, 10; 68:26; Ebr 2:12; Yn 20:17 Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu,
katika kusanyiko nitakusifu wewe.
23 #
Yer 3:17; Za 66:8; 33:2, 8; 103:1; 86:12; 106:1; 50:15; 113:1; 117:1; 135:19; Isa 24:15; 25:3; 49:23; 60:9; Kum 14:23 Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni!
Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye!
Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!
24 #
Ebr 5:7; Za 9:12; 102:17; 13:1; 27:9; 69:17; 102:2; 143:7; Ay 24:12; 36:5 Kwa maana hakupuuza wala kudharau
mateso ya aliyeonewa;
hakumficha uso wake
bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.
25 #
Za 26:12; 35:18; 40:9; 82:1; Hes 30:2 Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa,
nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe.
26 #
Za 107:9; 40:16 Maskini watakula na kushiba,
wale wamtafutao Bwana watamsifu:
mioyo yenu na iishi milele!
27 #
Za 2:8; 86:9; 102:22; Dan 7:27; Mik 4:1 Miisho yote ya dunia itakumbuka
na kumgeukia Bwana,
nazo jamaa zote za mataifa
watasujudu mbele zake,
28 #
Za 47:7; Zek 14:9; Mt 6:13 kwa maana ufalme ni wa Bwana
naye hutawala juu ya mataifa.
29 #
Za 45:12; 89:48; 95:6; 96:9; 99:5; Isa 26:19; 27:13; 49:7; 66:23; Zek 14:16 Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu.
Wote waendao mavumbini
watapiga magoti mbele yake,
wote ambao hawawezi
kudumisha uhai wao.
30 #
Isa 53:10; 54:3; 61:9; 66:22; Za 102:18 Wazao wa baadaye watamtumikia yeye;
vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.
31 #
Za 5:8; 71:18; 78:6; 40:9; 102:18; Lk 18:31; 24:44 Watatangaza haki yake kwa watu
ambao hawajazaliwa bado,
kwa maana yeye ametenda hili.