23
Zaburi 23
Bwana Mchungaji Wetu
Zaburi ya Daudi.
1 #
Mwa 48:15; Yn 10:11; Flp 4:19; Za 28:9; 34:9, 10; 84:11; 107:9; 1Pet 2:25 Bwana ndiye mchungaji wangu,
sitapungukiwa na kitu.
2 #
Eze 34:14; Ufu 7:17; Za 36:8; 46:4 Hunilaza katika malisho
ya majani mabichi,
kando ya maji matulivu huniongoza,
3 #
Isa 42:16; Za 5:8; 106:8; 19:7; 79:9; 25:9, 11; 73:24; 31:3; 109:21; 143:11 hunihuisha nafsi yangu.
Huniongoza katika njia za haki
kwa ajili ya jina lake.
4 #
Ay 3:5; Za 107:14; Isa 43:2; Za 3:6; 27:1; 16:8; 46:11; Isa 8:10; Zek 8:23; Mt 1:23; Mdo 18:9, 10 Hata kama nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.
5 #
Ay 36:16; Za 16:5; 45:7; 92:10; Lk 7:46 Waandaa meza mbele yangu
machoni pa adui zangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
kikombe changu kinafurika.
6 #
Neh 9:25; 2Kor 5:1 Hakika wema na upendo vitanifuata
siku zote za maisha yangu,
nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
milele.