Zaburi 24
NEN

Zaburi 24

24
Zaburi 24
Mfalme Mkuu
Zaburi ya Daudi.
1 # Kut 9:29; Ay 41:11; 1Kor 10:26 Dunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake,
ulimwengu, na wote waishio ndani yake,
2 # Za 104:3; Mwa 1:6; 2Pet 3:5 maana aliiwekea misingi yake baharini
na kuifanya imara juu ya maji.
3 # Za 2:6; 15:1; 65:4 Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana?
Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?
4 # 2Sam 22:21; Za 51:10; 73:1; Mt 5:8; Eze 18:15 Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,
yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake
au kuapa kwa kitu cha uongo.
5 # Kum 11:26; Za 17:2 Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana,
na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.
6 # Za 27:8; 105:4; 119:58; Hos 5:15 Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao,
wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
7 # Isa 26:2; 60:11, 18; 62:10; Za 74:12; 29:3; 118:19, 20; 44:4; Mdo 7:2; 1Kor 2:8; Zek 9:9; Mt 21:5; Hag 2:7; Mal 3:1 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
inukeni enyi milango ya kale,
ili mfalme wa utukufu apate kuingia.
8 # 1Nya 29:11; Za 89:13; Kum 4:34; Yer 50:34; Efe 6:10; Kut 15:3, 6 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Bwana aliye na nguvu na uweza,
ni Bwana aliye hodari katika vita.
9Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
viinueni juu enyi milango ya kale,
ili Mfalme wa utukufu apate kuingia.
10 # 1Sam 1:11 Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Bwana Mwenye Nguvu Zote;
yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014