Zaburi 25
NEN

Zaburi 25

25
Zaburi 25#25 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Kumwomba Mungu Uongozi Na Ulinzi
Zaburi ya Daudi.
1 # Za 86:4; 143:8 Kwako wewe, Ee Bwana,
nainua nafsi yangu,
2 # Za 31:6; 143:8 ni wewe ninayekutumainia,
Ee Mungu wangu.
Usiniache niaibike,
wala usiache adui zangu wakanishinda.
3 # Za 22:5; 2Tim 3:4; Isa 29:22; 24:16; Hab 1:13; Sef 3:4 Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea
atakayeaibishwa,
bali wataaibishwa
wafanyao hila bila sababu.
4 # Ay 34:32 Nionyeshe njia zako, Ee Bwana,
nifundishe mapito yako,
5 # Za 31:3; 43:3; Yn 16:13 niongoze katika kweli yako na kunifundisha,
kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,
nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.
6 # Za 5:7; 98:3; Isa 63:7, 15; Yer 31:20; Hos 11:8 Kumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo,
kwa maana zimekuwepo tangu zamani.
7 # Ay 13:26; Isa 54:4; Yer 3:25; 31:19; 32:30; 2Tim 2:22; Eze 16:22, 60; 23:3; Za 34:8; 83:1; 107:17; 6:4; 51:1; 69:16; 109:26; 119:124; Kut 3:21; 1Nya 16:34 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu
wala njia zangu za uasi,
sawasawa na upendo wako unikumbuke,
kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana.
8 # Za 32:8; 92:15; Isa 26:7; 28:26 Bwana ni mwema na mwenye adili,
kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.
9 # Za 23:3, 4; 18:25; 103:18; 132:12 Huwaongoza wanyenyekevu katika haki,
naye huwafundisha njia yake.
10 # Za 18:25; 103:18; 132:12 Njia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu
kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake.
11 # Kut 9:16; Za 31:3; 79:9; 34:9; Kut 32:30; Za 78:38; Yer 14:7 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako,
unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi.
12 # Ay 1:8 Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana?
Atamfundisha katika njia
atakayoichagua kwa ajili yake.
13 # Kum 30:15; Mt 5:5; Ay 8:7; 1Fal 3:14; Hes 14:24 Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake,
nao wazao wake watairithi nchi.
14 # Mit 3:32; Yn 7:17; Mwa 17:2 Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao,
yeye huwajulisha agano lake.
15 # 2Nya 20:12; Za 119:110; 123:2; Ebr 12:2; Ay 34:30 Macho yangu humwelekea Bwana daima,
kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa
miguu yangu kutoka mtego.
16 # Hes 6:25; Za 6:4; 68:6 Nigeukie na unihurumie,
kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka.
17 # 1Fal 1:29; Za 6:3; 39:2; 34:6, 17; 40:12; 54:7; 116:3 Shida za moyo wangu zimeongezeka,
niokoe katika dhiki yangu.
18 # Za 13:3; Rum 12:12; 2Sam 16:12 Uangalie mateso na shida zangu
na uniondolee dhambi zangu zote.
19 # Za 3:1; 9:13; 69:4; 35:19 Tazama adui zangu walivyo wengi,
pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!
20 # Za 2:12; 86:2; 17:13; 22:21; 43:1; 71:2; 116:4; 140:1; 142:6; 144:11 Uyalinde maisha yangu na uniokoe,
usiniache niaibike,
kwa maana nimekukimbilia wewe.
21 # Mwa 20:5; Mal 2:6; Mit 10:9; 1Fal 9:4; Za 88:10; 111:8; Isa 60:17 Uadilifu na uaminifu vinilinde,
kwa sababu tumaini langu ni kwako.
22 # Za 103:8; Lk 24:21 Ee Mungu, wakomboe Israeli,
katika shida zao zote!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014