26
Zaburi 26
Maombi Ya Mtu Mwema
Zaburi ya Daudi.
1 #
1Sam 24:15; Isa 12:2; 25:9; Mit 20:7; Yer 17:7; Za 15:2; 22:4; 40:4; 2Fal 20:3; Dan 3:28; Ebr 10:23 Ee Bwana, nithibitishe katika haki,
maana nimeishi maisha yasiyo na lawama;
nimemtumainia Bwana
bila kusitasita.
2 #
Za 7:9; 66:10; Kum 6:6; Eze 11:5; Yer 22:20; 20:12 Ee Bwana, unijaribu, unipime,
uuchunguze moyo wangu
na mawazo yangu;
3 #
1Fal 2:4; Za 6:4; 40:11; 43:3; 86:11; 119:30 kwa maana upendo wako
uko mbele yangu daima,
nami natembea siku zote
katika kweli yako.
4 #
Za 1:1; 28:3; Mt 6:2 #
Amo 9:6; Zek 10:1 Siketi pamoja na watu wadanganyifu,
wala siandamani na wanafiki,
5 #
Za 139:21
ninachukia kusanyiko la watenda mabaya
na ninakataa kuketi pamoja na waovu.
6 #
Za 73:13; Mt 27:24 Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia,
naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana,
7 #
Isa 42:12; 60:6; Yos 3:5; Za 9:1 nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa,
huku nikisimulia matendo yako ya ajabu.
8 #
Za 96:6; 122:6; Isa 66:10; 2Nya 7:1; Kut 29:43 Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi,
mahali ambapo utukufu wako hukaa.
9 #
Za 5:6; 28:3; 55:23; 139:19; Mit 29:10 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi,
wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu,
10 #
Za 21:11; Isa 1:23; Ay 36:18; Eze 22:12 ambao mikononi mwao kuna mipango miovu,
ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa.
11 #
Za 31:5; 69:18; 119:134; Tit 2:14 Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama;
nikomboe na unihurumie.
12 #
Za 22:25; 27:11; Ay 36:18; Lk 6:17; Isa 26:7; 40:3-4; 45:13; Zek 4:7 Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare;
katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana.