Zaburi 27
NEN

Zaburi 27

27
Zaburi 27
Sala Ya Kusifu
Zaburi ya Daudi.
1 # 2Sam 22:29; Ay 13:5; Za 3:8; 9:9; 56:4, 11; 118:6; Kut 15:2 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,
nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu,
nimhofu nani?
2 # Za 9:3; 20:8; 37:24; Dan 11:19; Rum 11:11 Waovu watakaposogea dhidi yangu
ili wanile nyama yangu,
adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia,
watajikwaa na kuanguka.
3 # Mwa 4:7; Za 3:6; Ay 4:6 Hata jeshi linizunguke pande zote,
moyo wangu hautaogopa;
hata vita vitokee dhidi yangu,
hata hapo nitakuwa na ujasiri.
4 # Lk 10:42; Za 23:6; 61:4 Jambo moja ninamwomba Bwana,
hili ndilo ninalolitafuta:
niweze kukaa nyumbani mwa Bwana
siku zote za maisha yangu,
niutazame uzuri wa Bwana
na kumtafuta hekaluni mwake.
5 # Ay 38:23; Za 12:7, 8; 40:2 Kwa kuwa siku ya shida,
atanihifadhi salama katika maskani yake,
atanificha uvulini mwa hema yake
na kuniweka juu kwenye mwamba.
6 # 2Sam 22:49; Za 3:3; 33:2; 54:6; 18:48; 22:12; 92:1; 50:14; 107:22; 116:17; 147:7; Ezr 3:13; Ay 22:26; Kut 15:1; Efe 5:19 Kisha kichwa changu kitainuliwa
juu ya adui zangu wanaonizunguka.
Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe;
nitamwimbia Bwana na kumsifu.
7 # Za 4:1; 5:3; 18:6; 55:17; 119:149; 130:2; Isa 28:23 Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana,
unihurumie na unijibu.
8 # 1Nya 16:11 Moyo wangu unasema kuhusu wewe,
“Utafute uso wake!”
Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”
9 # Za 2:5; 119:8; 18:46; 22:24; 37:28; Mwa 49:25; Kum 31:17; 33:29; 4:31; Isa 41:17; 62:12; Yer 14:9 Usinifiche uso wako,
usimkatae mtumishi wako kwa hasira;
wewe umekuwa msaada wangu.
Usinikatae wala usiniache,
Ee Mungu Mwokozi wangu.
10Hata kama baba yangu na mama wakiniacha,
Bwana atanipokea.
11 # Ezr 8:21; Za 5:8; 72:4; 78:42; 106:10; Yer 21:12; Kut 33:13 Nifundishe njia yako, Ee Bwana,
niongoze katika njia iliyonyooka
kwa sababu ya watesi wangu.
12 # Kum 19:16; Mt 26:60; Mdo 6:13; 1Kor 15:15 Usiniachilie kwa nia za adui zangu,
kwa maana mashahidi wa uongo
wameinuka dhidi yangu,
wakipumua ujeuri.
13 # Kut 33:19; 2Nya 6:41; Za 33:6; 31:19; 145:7; Ay 18:13 Nami bado nina tumaini hili:
nitauona wema wa Bwana
katika nchi ya walio hai.
14 # Efe 6:10; Amu 5:21; Kum 1:21; Sef 3:8; Hab 2:3; Za 33:20; 130:5, 6; Mdo 1:4; Isa 8:17; 30:18 Mngojee Bwana,
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
nawe, umngojee Bwana.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014