Zaburi 28
NEN

Zaburi 28

28
Zaburi 28
Kuomba Msaada
Zaburi ya Daudi.
1 # Kum 1:45; Es 4:14; Ay 33:18 Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu;
usiwe kwangu kama kiziwi.
Kwa sababu ukinyamaza
nitafanana na walioshuka shimoni.
2 # Za 17:1; 61:1; 5:7; 11:4; 116:1; 63:4; 130:2; 142:1; 143:1; 141:2; Mao 2:19; Ezr 9:5; 1Tim 2:8 Sikia kilio changu unihurumie
ninapokuita kwa ajili ya msaada,
niinuapo mikono yangu kuelekea
Patakatifu pa Patakatifu pako.
3 # Za 12:2; 26:4; 55:21; Yer 9:8 Usiniburute pamoja na waovu,
pamoja na hao watendao mabaya,
ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri,
lakini mioyoni mwao wameficha chuki.
4 # Za 62:12; 2Tim 4:14; Mao 3:64; Ufu 18:6; 22:12 Walipe sawasawa na matendo yao,
sawasawa na matendo yao maovu;
walipe sawasawa na kazi za mikono yao,
uwalipe wanavyostahili.
5 # Isa 5:12 Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana,
na yale ambayo mikono yake imetenda,
atawabomoa na kamwe
hatawajenga tena.
6 # Mwa 24:27; Efe 1:3; 2Kor 1:3; 1Pet 1:3 Bwana asifiwe,
kwa maana amesikia kilio changu
nikimwomba anihurumie.
7 # Za 144:9; 13:5; 16:9; 33:3; 40:3; 69:30; 149:1; 18:1; 112:7; Isa 26:3; Kum 16:15 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,
moyo wangu umemtumaini yeye,
nami nimesaidiwa.
Moyo wangu unarukaruka kwa furaha
nami nitamshukuru kwa wimbo.
8 # Za 18:1; 27:1; 20:6; Kut 15:2; Hab 3:13 Bwana ni nguvu ya watu wake,
ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.
9 # Za 78:52, 71; 80:1; 106:47; 118:25; 23:1; 1Nya 6:35; 11:2; Kut 34:9; Isa 40:11; 46:3; 63:9; Eze 34:12; Yer 31:10; Mik 7:14; Kum 1:31; 32:11 Waokoe watu wako na uubariki urithi wako;
uwe mchungaji wao na uwabebe milele.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014