29
Zaburi 29
Sauti Ya Bwana Wakati Wa Dhoruba
Zaburi ya Daudi.
1 #
1Nya 16:28; 2Sam 1:19; Isa 10:13; Za 103:20; 8:1 Mpeni Bwana, enyi mashujaa,
mpeni Bwana utukufu na nguvu.
2 #
1Nya 16:29; Za 96:7-9 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;
mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
3 #
Ay 37:5; Za 24:7; 18:13; 46:6; 68:33; 77:17; Mdo 7:2; 1Sam 2:10; Yer 10:13; 25:30; Yoe 2:11; Amo 1:2; Kut 15:10 Sauti ya Bwana iko juu ya maji;
Mungu wa utukufu hupiga radi,
Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.
4 #
Za 68:33
Sauti ya Bwana ina nguvu;
sauti ya Bwana ni tukufu.
5 #
Amu 9:15
Sauti ya Bwana huvunja mierezi;
Bwana huvunja vipande vipande
mierezi ya Lebanoni.
6 #
Za 92:10; 114:4; Kum 3:9; Ay 39:9; Hes 23:22 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,
Sirioni#29:6 Yaani Mlima Hermoni. urukaruke kama mwana nyati.
7 #
Eze 1:14; Ufu 8:5 Sauti ya Bwana hupiga kwa miali
ya umeme wa radi.
8 #
Hes 13:26; 20:1 Sauti ya Bwana hutikisa jangwa;
Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
9 #
Isa 2:13; Eze 27:6; Amo 2:9; Za 26:8 Sauti ya Bwana huzalisha ayala,
na huuacha msitu wazi.
Hekaluni mwake wote wasema,
“Utukufu!”
10 #
Mwa 6:17; Kut 15:18 Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;
Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.
11 #
Za 18:1; 28:8; 68:35; Law 26:6; Hes 6:26; Isa 40:29 Bwana huwapa watu wake nguvu;
Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.