Zaburi 30
NEN

Zaburi 30

30
Zaburi 30
Maombi Ya Shukrani
Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.
1 # Kut 15:2; Isa 14:15; Ay 11:8; Mit 9:18; Za 63:9; 107:26; 22:17 Nitakutukuza wewe, Ee Bwana,
kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,
na hukuacha adui zangu
washangilie juu yangu.
2 # Za 5:2; 88:13; 6:2-4; Hes 12:13 Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie
na wewe umeniponya.
3 # Za 40:1, 2; 16:10; 56:13; 28:1; 55:23; 69:15; 86:13; 143:7; Mit 1:12; Isa 38:17; Yon 2:6 Ee Bwana, umenitoa Kuzimu,
umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.
4 # Za 33:1; 47:7; 68:4; 16:3; 33:21; 103:1; 145:21; Kut 3:15 Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;
lisifuni jina lake takatifu.
5 # Za 103:9; 126:6; 6:6; 2Sam 15:30; 2Kor 4:17; Ezr 3:1; Ay 14:13; Yer 31:6 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,
bali upendo wake hudumu siku zote.
Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,
lakini asubuhi kukawa na furaha.
6 # Ay 29:18 Nilipofanikiwa nilisema,
“Sitatikiswa kamwe.”
7 # Kum 31:17; Za 104:29 Ee Bwana, uliponijalia,
uliuimarisha mlima wangu,
lakini ulipouficha uso wako
nilifadhaika.
8Kwako wewe, Ee Bwana, niliita,
kwa Bwana niliomba rehema:
9 # Ay 33:18; Isa 38:18; Za 6:5; 88:11; 115:17 “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu?
Katika kushuka kwangu shimoni?
Je, mavumbi yatakusifu?
Je, yatatangaza uaminifu wako?
10 # Za 17:1; 4:1; 20:2 Ee Bwana, unisikie na kunihurumia,
Ee Bwana, uwe msaada wangu.”
11 # 2Sam 3:31; 6:14; Es 4:1; Kut 15:20; Za 35:13; 16:9; Kum 16:15 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,
ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,
12 # Za 35:18; 75:1; 118:21; 44:8; 52:9; Ufu 11:17 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.
Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014