31
Zaburi 31
Maombi Na Sifa Kwa Kuokolewa Kutoka Kwa Adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 7:1; 5:8 Ee Bwana, nimekukimbilia wewe,
usiache nikaaibika kamwe,
kwa haki yako uniokoe.
2 #
Za 6:4
Nitegee sikio lako,
uje uniokoe haraka;
uwe kwangu mwamba wa kimbilio,
ngome imara ya kuniokoa.
3 #
Za 18:2; 23:3; Yer 14:7 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,
uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.
4 #
1Sam 28:9; Ay 18:10; Za 9:9 Uniepushe na mtego niliotegewa,
maana wewe ndiwe kimbilio langu.
5 #
Lk 23:46; Ebr 6:18; Mdo 7:59; Isa 45:19; 65:16; 2Tim 1:12 Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako,
unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli.
6 #
Kum 32:21; Za 4:5 Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili;
mimi ninamtumaini Bwana.
7 #
Yn 10:27; Lk 22:44; Za 25:17 Nitafurahia na kushangilia upendo wako,
kwa kuwa uliona mateso yangu
na ulijua maumivu ya nafsi yangu.
8 #
Za 18:19; Kum 32:30; 2Sam 22:20 Hukunikabidhi kwa adui yangu
bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi.
9 #
Za 4:1; 6:7; 63:1 Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida;
macho yangu yanafifia kwa huzuni,
nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko.
10 #
Za 6:6; 22:5; 32:4; 38:10; 73:26; 25:18; 6:2 Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi,
naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali;
nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso,
na mifupa yangu inachakaa.
11 #
Kum 30:7; Za 3:7; 25:19; 102; 22:6; 38:11; 88:8 Kwa sababu ya adui zangu wote,
nimedharauliwa kabisa na jirani zangu,
hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho,
wale wanionao barabarani hunikimbia.
12 #
Za 28:1; 88:4 Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa,
nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika.
13 #
Law 19:16; Isa 13:8; Za 50:20; 41:7; 56:6; 71:10; 83:3; Ay 18:11; Yer 6:25; 20:3, 10; 46:5; 49:5; Mao 2:22; Mwa 37:18; Mt 12:14; 27:1 Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi;
vitisho viko pande zote;
kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu,
na kula njama kuniua.
14 #
Za 4:5
Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana;
nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”
15 #
Ay 14:5
Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,
uniokoe mikononi mwa adui zangu
na wale wanifuatiao.
16 #
Hes 6:25; Dan 9:17; Za 4:6; 6:4 Mwangazie mtumishi wako uso wako,
uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma.
17 #
Za 22:5; 94:17; 115:17; 25:2; 1Sam 2:9 Usiniache niaibike, Ee Bwana,
kwa maana nimekulilia wewe,
bali waovu waaibishwe
na kunyamazishwa Kuzimu.
18 #
Za 120:2; 12:3; Mit 10:18; 26:24; 1Sam 2:3; Yud 15 Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe,
kwa maana kwa kiburi na dharau
wao husema kwa majivuno
dhidi ya wenye haki.
19 #
Za 27:13; 23:5; Isa 64:4; 1Kor 2:9; Rum 11:22 Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,
uliowawekea akiba wakuchao,
ambao huwapa wale wakukimbiliao
machoni pa watu.
20 #
Za 55:8; 27:5; 17:8; Mwa 37:18; Ay 5:21 Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako
kutokana na hila za wanadamu;
katika makao yako huwaweka salama
kutokana na ndimi za mashtaka.
21 #
Za 28:6; 17:7; 1Sam 23:7 Atukuzwe Bwana,
kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu
nilipokuwa katika mji uliozingirwa.
22 #
Za 116:11; 37:9; 88:5; 6:9; 66:19; 116:1; 145:19; Ay 6:9; 17:1; Isa 38:12 Katika hofu yangu nilisema,
“Nimekatiliwa mbali na macho yako!”
Hata hivyo ulisikia kilio changu
ukanihurumia nilipokuita unisaidie.
23 #
Za 4:3; 94:2; 18:25; Ufu 2:10; Kum 32:41; 1Pet 1:5 Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote!
Bwana huwahifadhi waaminifu,
lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.
24 #
Za 27:14
Kuweni hodari na mjipe moyo,
ninyi nyote mnaomtumaini Bwana.