Zaburi 33
NEN

Zaburi 33

33
Zaburi 33
Ukuu Na Wema Wa Mungu
1 # Za 64:10; 101:1; 147:1; 11:7 Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki;
kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
2 # Mwa 4:21; 1Kor 14:7; Ufu 5:8; Za 92:3; 144:9 Msifuni Bwana kwa kinubi,
mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.
3 # Za 40:3; 35:27; 47:1; Isa 42:10; Ufu 5:9; Ay 3:7 Mwimbieni wimbo mpya;
pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.
4 # Ufu 19:9; 22:6; Za 19:8; 18:25; 119:142; 25:10 Maana neno la Bwana ni haki na kweli,
ni mwaminifu kwa yote atendayo.
5 # Za 11:7; 6:4 Bwana hupenda uadilifu na haki;
dunia imejaa upendo wake usiokoma.
6 # Ebr 11:3; Kut 8:19; Mwa 1:3, 16; 2Nya 2:12; Yn 1:1-3; Ay 26:13 Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa,
jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.
7 # Mwa 1:10; Yos 3:16 Ameyakusanya maji ya bahari
kama kwenye chungu;
vilindi vya bahari
ameviweka katika ghala.
8 # Kum 6:13; 14:23; Za 2:11; 49:1; Isa 18:3; Mik 1:2 Dunia yote na imwogope Bwana,
watu wote wa dunia wamche.
9 # Za 148:5; Mwa 1:3 Kwa maana Mungu alisema, na ikawa,
aliamuru na ikasimama imara.
10 # Isa 44:25; Za 2:1; Ay 5:12 Bwana huzuia mipango ya mataifa,
hupinga makusudi ya mataifa.
11 # Hes 23:19; Yer 51:12, 29; Ay 23:13; Mit 19:21; Eze 38:10; Mdo 4:27, 28 Lakini mipango ya Bwana inasimama imara milele,
makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.
12 # Za 144:15; 65:4; 4:3; 84:4; Kum 7:6; Kut 8:22; 34:9 Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake.
13 # Za 53:2; 102:19; 11:4; 14:2; Ebr 4:13; 2Nya 16:9; Ay 28:24 Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini
na kuwaona wanadamu wote;
14 # Law 15:31; 1Fal 8:39 kutoka maskani mwake huwaangalia
wote wakaao duniani:
15 # Ay 10:8; 11:11; 10:4; Yer 32:19; Isa 64:8; Hes 7:2; Za 44:21; 119:73; Mit 24:12 yeye ambaye huumba mioyo yao wote,
ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.
16 # 1Sam 14:6 Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake;
hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake.
17 # Za 20:7 Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu,
licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa.
18 # Kut 3:16; Ay 36:7; Za 11:4; 6:4; 34:15; 1Pet 3:12 Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao,
kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,
19 # Za 56:13; Ay 5:20; Mdo 12:11 ili awaokoe na mauti,
na kuwahifadhi wakati wa njaa.
20 # Za 27:14 Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini,
yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
21 # 1Sam 2:1; Yoe 2:23; Za 30:4; 99:3 Mioyo yetu humshangilia,
kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.
22 # Za 6:4 Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana,
tunapoliweka tumaini letu kwako.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014