34
Zaburi 34#34 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Sifa Na Wema Wa Mungu
Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka.
1 #
Za 71:6; Efe 5:20; 1The 5:18 Nitamtukuza Bwana nyakati zote,
sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
2 #
Za 44:8; 69:32; 107:42; 119:74; Yer 9:24; 1Kor 1:31 Nafsi yangu itajisifu katika Bwana,
walioonewa watasikia na wafurahi.
3 #
Za 63:3; 86:12; Dan 4:37; Kut 15:2; Yn 17:1; Rum 15:6 Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
4 #
Za 18:6; 77:2; 18:43; 22:4; 56:13; 86:13; Kut 32:11; Yon 2:2; Mt 7:7; Lk 11:9 Nilimtafuta Bwana naye akanijibu,
akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
5 #
Kut 34:29; Za 25:3; 44:15; 69:7; 83:16 Wale wamtazamao hutiwa nuru,
nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
6 #
Za 25:17; 2Sam 22:1 Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia,
akamwokoa katika taabu zake zote.
7 #
Mwa 32:1; Ebr 1:14; Dan 3:28; 6:22; Mt 18:10; Isa 31:5; Za 22:4; 37:40; 41:1; 97:10; Mdo 12:11; 2Fal 16:17 Malaika wa Bwana hufanya kituo
akiwazunguka wale wamchao,
naye huwaokoa.
8 #
Ebr 6:5; 1Pet 2:3; Za 2:12 Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema,
heri mtu yule anayemkimbilia.
9 #
Flp 4:19; Za 23:1; Kum 6:13; Ufu 14:7 Mcheni Bwana enyi watakatifu wake,
kwa maana wale wamchao
hawapungukiwi na chochote.
10 #
Za 23:1
Wana simba wenye nguvu
hutindikiwa na kuona njaa,
bali wale wamtafutao Bwana
hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
11 #
Za 66:16; 32:8; 19:9 Njooni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumcha Bwana.
12 #
Mhu 3:13; 1Pet 3:10 Yeyote kati yenu anayependa uzima
na kutamani kuziona siku nyingi njema,
13 #
1Pet 2:22; Za 39:1; 141:3; Mit 13:3; 21:23; Yak 1:26; Za 12:2 basi auzuie ulimi wake na mabaya,
na midomo yake kutokana na kusema uongo.
14 #
Za 37:27; Isa 1:17; 3Yn 11; Rum 14:19 Aache uovu, atende mema,
aitafute amani na kuifuatilia.
15 #
Ay 36:7; 23:10; Mal 3:16; Yn 9:31; Za 33:18 Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
16 #
Law 17:10; Za 9:6; Yer 23:30; 44:11; Mit 10:7; Kut 17:14; 1Pet 3:10-12 Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu,
ili kufuta kumbukumbu lao duniani.
17 #
Za 145:19
Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia,
huwaokoa katika taabu zao zote.
18 #
Kum 4:7; Za 51:17; 119:151; 145:18; 109:16; 147:3; Isa 50:8; 61:1 Bwana yu karibu na waliovunjika moyo,
na huwaokoa waliopondeka roho.
19 #
Za 34:17; 25:17; Ay 5:19; 2Tim 3:11 Mwenye haki ana mateso mengi,
lakini Bwana humwokoa nayo yote,
20 #
Yn 19:34
huhifadhi mifupa yake yote,
hata mmoja hautavunjika.
21 #
Za 7:9; 9:16; 37:20; 73:27; 94:23; 106:43; 112:10; 140:11; Mit 14:32; 24:16 Ubaya utamuua mtu mwovu,
nao adui za mwenye haki watahukumiwa.
22 #
Kut 6:6; 15:13; Lk 1:68; Ufu 14:3; Za 2:12; 103:4; 2Sam 4:9 Bwana huwakomboa watumishi wake,
yeyote anayemkimbilia yeye
hatahukumiwa kamwe.