Zaburi 35
NEN

Zaburi 35

35
Zaburi 35
Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui
Zaburi ya Daudi.
1 # 1Sam 24:15; Kut 14:14 Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami,
upigane na hao wanaopigana nami.
2 # Za 3:3, 7; Ay 17:3; Mwa 50:24; 35:3; Hes 25:7; Za 27:1; Yos 8:18 Chukua ngao na kigao.
Inuka unisaidie.
3Inua mkuki wako na fumo#35:3 Fumo ni sawa na sagai, maana yake ni mkuki mfupi. lako
dhidi ya hao wanaonifuatia.
Iambie nafsi yangu,
“Mimi ni wokovu wako.”
4 # Za 38:12; 40:14; 69:6, 19; 70:2; 83:17; 25:3; 129:5; Yer 4:30; Mal 2:9; Isa 45:16 Wafedheheshwe na waaibishwe
wale wanaotafuta uhai wangu.
Wanaofanya shauri kuniangamiza
warudishwe nyuma kwa hofu.
5 # Ay 13:25; Za 1:4; 34:7 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
malaika wa Bwana akiwafukuza.
6Njia yao na iwe giza na ya utelezi,
malaika wa Bwana akiwafuatilia.
7 # Ay 18:8; 9:31; Za 7:4; 7:15; 55:23 Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu,
na bila sababu wamenichimbia shimo,
8 # Isa 47:11; 1The 5:3; Za 7:15; Mit 5:22 maafa na yawapate ghafula:
wavu walionifichia na uwatege wenyewe,
na waanguke katika shimo hilo,
kwa maangamizo yao.
9 # Za 2:11; 9:14; 13:5; 27:1; Lk 1:47; 1Sam 2:1; Isa 61:10; Ebr 3:18 Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana
na kuufurahia wokovu wake.
10 # Kut 9:14; Za 12:5; 71:19; 18:17, 31; 113:5; 37:14; 86:1; 74:21; 109:16; 140:12; Isa 41:17 Nitapaza sauti yangu nikisema,
“Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana?
Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao,
maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!”
11 # Kut 23:1; Mt 26:60 Mashahidi wakatili wanainuka,
wananiuliza mambo nisiyoyajua.
12 # Yer 18:20; Za 38:20; 109:5; Mit 17:13 Wananilipa baya kwa jema
na kuiacha nafsi yangu ukiwa.
13 # 2Sam 3:31; 1Fal 20:31; Za 30:11; 69:10, 11; 109:24; Ay 30:25 Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia
na nikajinyenyekesha kwa kufunga.
Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa,
14 # Za 38:6; 42:9; 43:2 niliendelea kuomboleza
kama vile wao ni rafiki au ndugu.
Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni
kama ninayemwombolezea mama yangu.
15 # Ay 31:29; 16:10 Lakini nilipojikwaa,
walikusanyika kwa shangwe;
washambuliaji walijikusanya dhidi yangu
bila mimi kujua.
Walinisingizia pasipo kukoma.
16 # Za 22:7; Mk 10:34; 9:18; Ay 16:9; Mdo 7:54 Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki,
wamenisagia meno.
17 # Za 6:3; 22:20, 21; 57:4; 58:6 Ee Bwana, utatazama mpaka lini?
Niokoe maisha yangu na maangamizi yao,
uhai wangu wa thamani
kutokana na simba hawa.
18 # Za 22:20, 25; 42:4; 109:30 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,
nitakusifu katikati ya watu wengi.
19 # Za 9:13; 38:19; 69:4; Yn 15:25; Mit 6:13; 10:10 Usiwaache wale wanaonisimanga,
wale ambao ni adui zangu bila sababu;
usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu
wakonyeze jicho kwa hila.
20 # Za 38:12; 55:21; Yer 9:8; Mik 6:12 Hawazungumzi kwa amani,
bali wanatunga mashtaka ya uongo
dhidi ya wale wanaoishi
kwa utulivu katika nchi.
21 # Ay 16:10; Eze 25:3; Za 40:15; 70:3 Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha!
Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.”
22 # Kut 3:7; Za 10:1, 14 Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya.
Usiwe mbali nami, Ee Bwana.
23 # Za 7:6; 80:2; 17:13; 1Sam 24:15 Amka, inuka unitetee!
Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu.
24 # Za 22:17; 7:8; 26:11; 2The 1:6 Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu,
sawasawa na haki yako;
usiwaache wakusimange.
25 # Mit 1:12; Za 35:21; 124:3; Mao 2:16 Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!”
Au waseme, “Tumemmeza.”
26 # Za 22:17; 4:1; 109:29; 38:16; Ay 8:22; 19:5; Mik 7:10 Wote wanaofurahia dhiki yangu
waaibishwe na wachanganyikiwe;
hao wanaojiinua dhidi yangu
wavikwe aibu na dharau.
27 # Za 9:4; 20:5; 33:3; 147:11; 149:4; Ay 17:3 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki
wapige kelele za shangwe na furaha;
hebu waseme siku zote, “Bwana atukuzwe,
ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”
28 # Za 5:8; 51:14; 71:15, 24; 72:15 Ulimi wangu utanena haki yako
na sifa zako mchana kutwa.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014