Zaburi 36
NEN

Zaburi 36

36
Zaburi 36
Uovu Wa Mwanadamu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana.
1 # Ay 21:16; 23:15; Yer 2:19; 36:16, 24; Rum 3:18; Mit 8:13; Mwa 20:11; Mhu 12:3 Kuna neno moyoni mwangu
kuhusu hali ya dhambi ya mwovu.
Hakuna hofu ya Mungu
mbele ya macho yake.
2 # Kum 29:19 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno
hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake.
3 # Yer 4:22; 13:23; Za 10:7; 5:6, 9; 43:1; 144:8, 11; 94:8; Ay 5:13; Isa 44:20; Amo 3:10 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu,
ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.
4 # Mik 2:1; Rum 12:9; Isa 65:2; Za 52:3 Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya,
hujitia katika njia ya dhambi
na hakatai lililo baya.
5 # Za 89:1; 119:90; 108:4; 57:10; 89:2; 71:19; 103:11 Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni,
uaminifu wako hadi kwenye anga.
6 # Za 5:8; 68:15; Mwa 1:2; Za 104:14; 7:11; 145:9; Neh 9:6; Rum 11:33; Ay 7:20; 11:8 Haki yako ni kama milima mikubwa,
hukumu zako ni kama kilindi kikuu.
Ee Bwana, wewe huwahifadhi
mwanadamu na mnyama.
7 # Za 6:4; 17:8; 57:1; 91:4; Rut 2:12 Upendo wako usiokoma
ni wa thamani mno!
Watu wakuu na wadogo
hujificha uvulini wa mbawa zako.
8 # Za 65:4; 23:2; 63:5; Yer 31:12, 14; Ufu 22:1; Isa 25:6; Ay 20:17 Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako,
nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.
9 # Isa 12:3; 2:5; 9:2; 60:1, 19; Yer 2:13; Zek 13:1; Yn 1:4; 4:10, 14; Ufu 21:6; Mdo 26:18; Efe 5:8; Kol 1:13; 1Pet 2:9; Mit 10:11; 16:22; Za 87:7; 4:6; 27:1; 76:4; 104:2 Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,
katika nuru yako twaona nuru.
10 # Yer 31:3; 9:24; 22:16; Za 7:10; 11:2; 94:15; 125:4 Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe,
haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.
11 # Za 71:4; 140:4 Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu,
wala mkono wa mwovu usinifukuze.
12 # Za 18:38 Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka:
wametupwa chini, hawawezi kuinuka!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014