37
Zaburi 37#37 Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Mwisho Wa Mwovu Na Urithi Wa Mwenye Haki
Zaburi ya Daudi.
1 #
Mit 3:31; 3:17, 18; 24:19 Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu,
wala usiwaonee wivu watendao mabaya,
2 #
2Fal 19:26; Ay 14:2; Za 92:7; 102:4; 90:6; Yak 1:10; Isa 40:7; Za 37:38 kwa maana kama majani watanyauka mara,
kama mimea ya kijani watakufa mara.
3 #
Kum 30:20; Yn 10:9; Eze 34:14 Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema;
Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.
4 #
Ay 27:10; 7:6; Wim 2:3; Za 21:2; 145:19; Mit 6:33; Isa 58:14; 1Pet 1:8 Jifurahishe katika Bwana
naye atakupa haja za moyo wako.
5 #
Za 4:5; 57:10; Mt 6:25; 1Pet 5:7 Mkabidhi Bwana njia yako,
mtumaini yeye, naye atatenda hili:
6 #
Ay 11:8; 7:20; 11:17; Rum 11:33; Za 145:9; 18:24; 103:17; 112:3; Mik 7:9 Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko,
na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.
7 #
Kut 14:14; Yer 12:1; Isa 41:1; 38:13; Za 119:150; 40:1; 27:14; 21:11; 26:10; 130:5; Hab 3:16; Rum 8:25 Tulia mbele za Bwana
na umngojee kwa uvumilivu;
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,
wanapotekeleza mipango yao miovu.
8 #
Efe 4:26, 31; Ay 5:2; Kol 3:8; Mit 14:29; Za 73:3; Yak 1:19 Epuka hasira na uache ghadhabu,
usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.
9 #
Za 31:22; 101:8; 25:13; Mit 2:22; Isa 57:13; 40:31; 51:5, 22; 49:8, 23; 25:9; 26:8; Mt 5:5 Kwa maana waovu watakatiliwa mbali,
bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.
10 #
Ay 7:10; Eze 27:30 Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana,
ingawa utawatafuta, hawataonekana.
11 #
Hes 6:26; 14:24; Mt 5:5; Law 26:6 Bali wanyenyekevu watairithi nchi
na wafurahie amani tele.
12 #
Ay 16:9; Za 2:1; 31:13; 35:16; 112:10 Waovu hula njama dhidi ya wenye haki
na kuwasagia meno,
13 #
1Sam 26:10; Za 11:2; 35:10; 22:20; Eze 12:23 bali Bwana huwacheka waovu,
kwa sababu anajua siku yao inakuja.
14 #
Za 22:20; 11:2; 35:10 Waovu huchomoa upanga
na kupinda upinde,
ili wawaangushe maskini na wahitaji,
kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu.
15 #
1Sam 2:4; Yer 49:35; Za 9:16; 46:9 Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe,
na pinde zao zitavunjwa.
16 #
Mit 15:16; 16:8; 1Tim 6:6 Bora kidogo walicho nacho wenye haki
kuliko wingi wa mali wa waovu wengi;
17 #
Za 10:15; 41:12; 140:12; 145:14; 146:7; Ay 38:15 kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa,
lakini Bwana humtegemeza mwenye haki.
18 #
Ay 23:10; Za 44:21; 37:27, 29 Bwana anazifahamu siku za wanyofu,
na urithi wao utadumu milele.
19 #
Ay 5:20
Siku za maafa hawatanyauka,
siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.
20 #
Za 34:21; 68:2; 102:3; Isa 51:6 Lakini waovu wataangamia:
Adui za Bwana watakuwa
kama uzuri wa mashamba,
watatoweka,
watatoweka kama moshi.
21 #
Law 25:35; Za 112:5 Waovu hukopa na hawalipi,
bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.
22 #
Ay 5:3; Mit 3:33 Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi,
bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.
23 #
Za 66:9; 121:3; 7:9; 147:11; Mit 16:9; Hes 14:8; Ay 11:15 Kama Bwana akipendezwa na njia ya mtu,
yeye huimarisha hatua zake,
24 #
Za 13:4; 55:22; 119:165; 145:14; 38:17; 41:12; 27:2; Mit 3:23; 10:9; 2Nya 9:8 ajapojikwaa, hataanguka,
kwa maana Bwana
humtegemeza kwa mkono wake.
25 #
Mwa 15:1; Za 111:5; 145:15; Ebr 13:5; Mk 10:46 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,
lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa
au watoto wao wakiombaomba chakula.
26 #
Law 25:35; Kum 28:4; Za 112:2 Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti.
Watoto wao watabarikiwa.
27 #
Za 34:14; Yn 1:11; Hes 24:21 Acha ubaya na utende wema,
nawe utaishi katika nchi milele.
28 #
Za 11:7; 18:25; 97:10; Mwa 17:14; Kum 7:6; 32:26; Mit 2:22 Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki
naye hatawaacha waaminifu wake.
Watalindwa milele,
lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.
29 #
Mit 2:21; Isa 34:17 Wenye haki watairithi nchi,
na kuishi humo milele.
30 #
Za 49:3; Mit 10:13 Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima,
nao ulimi wake huzungumza lililo haki.
31 #
Kum 6:6; 32:35; Ay 22:22 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake;
nyayo zake hazitelezi.
32 #
Za 10:8; 11:5 Watu waovu huvizia wenye haki,
wakitafuta kuwaua;
33 #
Ay 32:3; 2Pet 2:9; Za 109:31; 34:22; 79:11; 2:9 lakini Bwana hatawaacha mikononi mwao
wala hatawaacha wahukumiwe
kuwa wakosa wanaposhtakiwa.
34 #
Za 27:14; 18:21; 52:6 Mngojee Bwana,
na uishike njia yake.
Naye atakutukuza uirithi nchi,
waovu watakapokatiliwa mbali,
utaliona hilo.
35 #
Ay 5:3
Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi
kama mwerezi wa Lebanoni,
36 #
Za 37:10; Dan 11:19; Mit 12:7; Isa 41:12 lakini alitoweka mara na hakuonekana,
ingawa nilimtafuta, hakupatikana.
37 #
Mwa 6:9; Za 11:7; 18:25; Isa 57:1-2 Watafakari watu wasio na hatia,
wachunguze watu wakamilifu,
kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.
38 #
Za 1:1, 2; 73:9, 19; Ay 1:1; 1The 4:17; Lk 2:25-30; Mdo 7:59, 60; 2Pet 1:14; Isa 32:17; 2Tim 4:6-8 Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa,
mafanikio yao yatakatiliwa mbali.
39 #
Isa 12:2; Yon 2:8; Za 3:8; 9:9 Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana,
yeye ni ngome yao wakati wa shida.
40 #
1Nya 5:20; Dan 3:17; Za 20:2; 18:48; 2:12; 34:7 Bwana huwasaidia na kuwaokoa,
huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi,
kwa maana wanamkimbilia.