Zaburi 38
NEN

Zaburi 38

38
Zaburi 38
Maombi Ya Mtu Anayeteseka
Zaburi ya Daudi. Maombi.
1 # Za 6:1 Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,
wala kuniadhibu katika ghadhabu yako.
2 # Ay 6:4 Kwa kuwa mishale yako imenichoma,
na mkono wako umenishukia.
3 # Mit 3:8; 4:22; Ay 33:19 Hakuna afya mwilini mwangu
kwa sababu ya ghadhabu yako,
mifupa yangu haina uzima
kwa sababu ya dhambi zangu.
4 # Za 40:12; 65:3; Hes 11:14; Ezr 9:6; Lk 11:46 Maovu yangu yamenifunika
kama mzigo usiochukulika.
5 # Za 147:3; Ay 19:17; Za 69:5; Mit 5:23; 12:23; 13:16; Mhu 10:3 Majeraha yangu yameoza na yananuka,
kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.
6 # Za 57:6; 145:14; 146:8; 35:14 Nimeinamishwa chini na kushushwa sana,
mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.
7 # Ay 14:22; 7:5 Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo,
hakuna afya mwilini mwangu.
8 # Za 6:3, 6; 22:1; 34:18; Mit 17:22; 5:11 Nimedhoofika na kupondwa kabisa,
nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni.
9 # Za 119:20; 143:7; Ay 3:24 Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku
yako wazi mbele zako,
kutamani kwangu sana
hakufichiki mbele zako.
10 # Ay 37:1; Za 6:7; 31:10; 19:8; 88:9 Moyo wangu unapigapiga,
nguvu zangu zimeniishia;
hata macho yangu yametiwa giza.
11 # Za 38:5; Lk 10:31 Rafiki na wenzangu wananikwepa
kwa sababu ya majeraha yangu;
majirani zangu wanakaa mbali nami.
12 # Za 35:4, 20; 140:5; 31:4; 141:9; 41:5 Wale wanaotafuta uhai wangu
wanatega mitego yao,
wale ambao wangetaka kunidhuru
huongea juu ya maangamizi yangu;
hufanya shauri la hila mchana kutwa.
13 # Za 115:6; 135:17; Isa 43:8; Mk 7:37 Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia,
ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake,
14nimekuwa kama mtu asiyesikia,
ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu.
15 # Za 27:14; 17:6; Yer 14:8 Ee Bwana, ninakungojea wewe,
Ee Bwana Mungu wangu, utajibu.
16 # Za 22:17; Kum 32:35 Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie,
wala wasijitukuze juu yangu
mguu wangu unapoteleza.”
17 # Za 37:24; 38:7; Ay 6:10 Kwa maana ninakaribia kuanguka,
na maumivu yangu yananiandama siku zote.
18 # Law 26:40; Ay 31:33; Za 32:5; Mit 28:13; 2Kor 7:9 Naungama uovu wangu,
ninataabishwa na dhambi yangu.
19 # Za 18:17; 25:19; 35:19 Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari,
wale wanaonichukia bila sababu ni wengi.
20 # Mwa 44:4; Yn 3:12; 1Pet 3:13; Za 54:5; 59:10; 119:23; 1Yn 3:12 Wanaolipa maovu kwa wema wangu
hunisingizia ninapofuata lililo jema.
21 # Za 22:1, 11; 27:9; 71:18; 119:8; 10:1; 35:22; 71:12 Ee Bwana, usiniache,
usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu.
22 # Za 22:19; 40:13; 1Nya 16:35; Kut 15:2; Isa 12:2 Ee Bwana Mwokozi wangu,
uje upesi kunisaidia.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014