39
Zaburi 39
Maombi Ya Mtu Anayeteseka
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.
1 #
1Fal 2:4; Kol 4:5; Ebr 2:1; Ay 1:22; 6:24; Yak 1:26; 3:2; Za 34:13; 119:9, 59; Mit 4:26, 27; 20:11 Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu
na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi;
nitaweka lijamu kinywani mwangu
wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”
2 #
Za 6:3; 25:17; 39:9; 77:4; 31:10; Ay 31:34 Lakini niliponyamaza kimya na kutulia,
hata pasipo kusema lolote jema,
uchungu wangu uliongezeka.
3 #
Yer 20:9; Lk 24:32; Za 1:2; 119:15; Yer 5:14; 20:9; 23:29 Moyo wangu ulipata moto ndani yangu,
nilipotafakari, moto uliwaka,
ndipo nikasema kwa ulimi wangu:
4 #
Ay 14:5; 14:2; 7:7; Mwa 47:9 “Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu
na hesabu ya siku zangu;
nijalie kujua jinsi maisha yangu
yanavyopita upesi.
5 #
Ay 10:20; 7:7; Za 62:9; 90:4; 89:45; 102:23 Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi;
muda wangu wa kuishi ni kama
hauna thamani kwako.
Maisha ya kila mwanadamu
ni kama pumzi.
6 #
Ay 8:9; 27:17; Mhu 6:12; Lk 12:20; Yak 4:14; 1:11; Za 102:11; 127:2 Hakika kila binadamu ni kama njozi
aendapo huku na huko:
hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili;
anakusanya mali nyingi,
wala hajui ni nani atakayeifaidi.
7 #
Za 9:18
“Lakini sasa Bwana, nitafute nini?
Tumaini langu ni kwako.
8 #
Isa 53:5, 8, 10; 43:28; Kum 28:37; Za 69:7; 51:1, 14; 32:1; 6:4; 79:4; Dan 9:16 Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote,
usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.
9 #
Za 38:13; Isa 38:15 Nilinyamaza kimya,
sikufumbua kinywa changu,
kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili.
10 #
2Nya 21:14; Eze 7:9; 24:16; Kut 9:3 Niondolee mjeledi wako,
nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako.
11 #
Kum 28:20; Isa 26:16; 51:8; 66:15; Eze 5:15; 2Pet 2:16; Za 94:10; 90:7; Ay 7:7; 13:28; Lk 12:33; Yak 5:2 Unakemea na kuadhibu wanadamu
kwa ajili ya dhambi zao;
unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo:
kila mwanadamu ni kama pumzi tu.
12 #
Za 17:1; 1Nya 29:15; Ebr 11:13; Law 25:23; Kum 1:45; 2Fal 20:5; Mwa 23:4; 47:9 “Ee Bwana, usikie maombi yangu,
usikie kilio changu unisaidie,
usiwe kiziwi kwa kulia kwangu.
Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni,
kama walivyokuwa baba zangu wote,
13 #
Ay 10:20, 21 Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena
kabla sijaondoka na nisiwepo tena.”