Zaburi 40
NEN

Zaburi 40

40
Zaburi 40
Wimbo Wa Sifa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Za 37:7; 116:1; 6:9; 31:22; 34:15; 7:15; 145:19 Nilimngoja Bwana kwa saburi,
naye akaniinamia, akasikia kilio changu.
2 # Ay 9:31; 30:19; Za 7:15; 69:14; 31:8; 27:5 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,
kutoka matope na utelezi;
akaiweka miguu yangu juu ya mwamba
na kunipa mahali imara pa kusimama.
3 # Za 28:7; 52:6; 64:9; Ufu 5:9; Kut 14:31 Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,
wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa
na kuweka tumaini lao kwa Bwana.
4 # Za 2:12; 34:8; 84:12; 101:5; 4:2; 138:6; Kum 31:20; Mit 3:34; 16:5; Isa 65:5; 1Pet 5:5 Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,
asiyewategemea wenye kiburi,
wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
5 # Kum 4:34; Isa 55:8; Za 75:1; 105:5; 136:4; 139:18; 71:15; 139:15 Ee Bwana Mungu wangu,
umefanya mambo mengi ya ajabu.
Mambo uliyopanga kwa ajili yetu
hakuna awezaye kukuhesabia;
kama ningesema na kuyaelezea,
yangekuwa mengi mno kuyaelezea.
6 # 1Sam 15:22; Isa 1:11; Hos 6:6; Yer 6:20; Mt 9:13; Amo 5:22; Kut 21:6; Za 50:8; 51:16 Dhabihu na sadaka hukuvitaka,
lakini umefungua masikio yangu;#40:6 Au: bali mwili uliniandalia.
sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi
hukuzihitaji.
7 # Ay 19:23; Yn 5:39; Yer 36:2; 45:1; Eze 2:9; Lk 24:44; Mdo 10:43; Ebr 10:7 Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja:
imeandikwa kunihusu katika kitabu.
8 # Mt 26:39; Yn 4:34; Ebr 10:5-7; Kum 6:6; Yer 15:16; Rum 7:22; Ay 22:22; 23:12 Ee Mungu wangu,
natamani kuyafanya mapenzi yako;
sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”
9 # Za 22:25, 31; 139:2; Yos 22:22 Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,
sikufunga mdomo wangu,
Ee Bwana, kama ujuavyo.
10 # Za 89:1; 22:22; Mdo 20:20; Flp 3:9; Rum 1:16, 17 Sikuficha haki yako moyoni mwangu;
ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.
Sikuficha upendo wako na kweli yako
mbele ya kusanyiko kubwa.
11 # Zek 1:12; Za 26:3; 61:7; 43:3; Mit 20:28 Ee Bwana, usizuilie huruma zako,
upendo wako na kweli yako daima vinilinde.
12 # Za 25:17; 38:4; 65:3; 69:4; 73:26 Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,
dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.
Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,
nao moyo unazimia ndani yangu.
13 # Za 22:19; 38:22 Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
14 # 1Sam 20:1; Es 9:2; Za 35:26; 35:4 Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
15 # Za 35:21 Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
wafadhaishwe na iwe aibu yao.
16 # Kum 4:29; 1Nya 28:9; Za 9:10; 119:2; 9:2; 35:27 Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
Bwana atukuzwe!”
17 # Neh 5:19; Mk 10:21; Za 86:1; 109:22; 144:3; 20:2; 18:2; 119:60 Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Bwana na anifikirie.
Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu;
Ee Mungu wangu, usikawie.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014