41
Zaburi 41
Maombi Ya Mtu Mgonjwa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Kum 14:29; Ay 24:4; Za 25:17; Mit 14:21; Mk 10:21 Heri mtu yule anayemjali mnyonge,
Bwana atamwokoa wakati wa shida.
2 #
Za 12:5; 32:7; 71:20; 119:88, 159; 138:7; 143:1; 37:22; Ezr 9:9; Kum 6:24 Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake,
atambariki katika nchi
na hatamwacha katika tamaa ya adui zake.
3 #
Za 6:6; 2Fal 1:4; 2Sam 13:5 Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani,
atamwinua kutoka kitandani mwake.
4 #
Za 6:2; 9:13; Kum 32:39; Za 51:4 Nilisema, “Ee Bwana nihurumie,
niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”
5 #
Za 38:12
Adui zangu wanasema kwa hila,
“Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.”
6 #
Za 12:2; 101:7; Mt 5:11; Mit 26:24; Law 19:16 Kila anapokuja mtu kunitazama,
huzungumza uongo,
huku moyo wake hukusanya masingizio;
kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.
7 #
Za 71:10
Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu,
hao huniwazia mabaya sana, wakisema,
8 #
2Fal 1:4
“Ugonjwa mbaya sana umempata,
kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”
9 #
Oba 1:7; Yn 13:18; 2Sam 15:12; Ay 19:14, 19; Hes 30:2; Lk 22:21; Za 55:20; 89:34; Mt 26:23 Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini,
yule aliyekula chakula changu
ameniinulia kisigino chake.
10 #
Za 3:3; 9:13; 2Sam 3:39 Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie,
ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.
11 #
Hes 14:8; Za 25:2 Najua kwamba wapendezwa nami,
kwa kuwa adui yangu hanishindi.
12 #
Za 21:6; 61:7; 34:15; 25:21; 18:35; 37:17; 63:8; Ay 4:7; Mdo 2:38 Katika uadilifu wangu unanitegemeza
na kuniweka kwenye uwepo wako milele.
13 #
Mwa 24:27; Za 72:18, 19; 89:52; 106:48 Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele.
Amen na Amen.