42
KITABU CHA PILI
(Zaburi 42–72)
Zaburi 42
Maombi Ya Mtu Aliye Uhamishoni
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.
1 #
Ay 19:27; Yoe 1:20; Za 18:33; 119:131; Kum 10:7 Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji,
ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu.
2 #
Za 43:4; 143:6; 84:7; 63:1; Yos 3:10; 1The 1:9; Yn 7:37; Rum 9:26; 1Sam 14:19; Mt 16:16; 9:26 Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai.
Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?
3 #
Ay 3:24; Mik 7:10; Za 79:10; 115:2; Yoe 2:17 Machozi yangu yamekuwa chakula changu
usiku na mchana,
huku watu wakiniambia mchana kutwa,
“Yuko wapi Mungu wako?”
4 #
1Sam 1:15; Isa 2:2; 30:29; Yon 2:9; Ezr 3:13; Yos 6:5; Za 35:18; 109:30; 55:14; 122:1; 95:2; 100:4; 147:7 Mambo haya nayakumbuka
ninapoimimina nafsi yangu:
Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu,
nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu,
kwa kelele za shangwe na za shukrani
katikati ya umati uliosherehekea.
5 #
Mao 3:20; Mt 26:38; Za 9:1; 38:6; 77:3; 25:5; 71:14; 56:3, 11; 18:46; Ay 20:2; Isa 50:10 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa sababu bado nitamsifu,
Mwokozi wangu na 6#Za 43:5; 63:6; 7:11; Mwa 13:10; Hes 13:29; Kum 3:8; 4:48Mungu wangu.
Nafsi yangu inasononeka ndani yangu;
kwa hiyo nitakukumbuka
kutoka nchi ya Yordani,
katika vilele vya Hermoni,
kutoka Mlima Mizari.
7 #
Eze 7:26; Mwa 1:2; 7:11; Za 69:2; Yon 2:3 Kilindi huita kilindi,
katika ngurumo za maporomoko ya maji yako;
mawimbi yako yote pamoja na viwimbi
vimepita juu yangu.
8 #
Za 57:3; 16:7; 133:3; Mhu 5:18; 8:15; Kum 28:8 Mchana Bwana huelekeza upendo wake,
usiku wimbo wake uko nami:
maombi kwa Mungu wa uzima wangu.
9 #
Za 18:31; 10:11; 35:14; 106:42; 9:13; 43:2; Ay 20:19 Ninamwambia Mungu Mwamba wangu,
“Kwa nini umenisahau?
Kwa nini niendelee kuomboleza,
nikiwa nimeonewa na adui?”
10 #
Za 89:51; 119:42; 44:16; 6:2; 102:8; Kum 32:27 Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali
adui zangu wanaponidhihaki,
wakiniambia mchana kutwa,
“Yuko wapi Mungu wako?”
11 #
Za 43:5
Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa sababu bado nitamsifu,
Mwokozi wangu na Mungu wangu.