Zaburi 43
NEN

Zaburi 43

43
Zaburi 43
Maombi Ya Mtu Aliyeko Uhamishoni Yanaendelea
1 # Amu 6:31; Za 25:20; 36:3; 109:2; 7:8 Ee Mungu unihukumu,
nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu,
niokoe na watu wadanganyifu na waovu.
2 # Za 44:9; 74:1; 88:14; 89:38; 35:14; 42:9; 28:7; Isa 26:4 Wewe ni Mungu ngome yangu.
Kwa nini umenikataa?
Kwa nini niendelee kuomboleza,
nikiwa nimeonewa na adui?
3 # Za 2:6; 3:4; 27:1; 26:3; 25:5; 2Sam 15:25 Tuma hima nuru yako na kweli yako
na viniongoze;
vinilete mpaka mlima wako mtakatifu,
mpaka mahali unapoishi.
4 # Za 42:2; 26:6; 84:3; 21:6; 16:3; Mwa 4:21 Ndipo nitakwenda madhabahuni pa Mungu,
kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu.
Nitakusifu kwa kinubi,
Ee Mungu, Mungu wangu.
5 # Za 42:5, 6, 11 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa sababu bado nitamsifu
Mwokozi wangu na Mungu wangu.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014