Zaburi 44
NEN

Zaburi 44

44
Zaburi 44
Kuomba Ulinzi Wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.
1 # 2Sam 7:22; 1Nya 17:20; Yer 26:11; Amu 6:13; Kum 32:7; Ay 37:23 Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu,
baba zetu wametueleza
yale uliyotenda katika siku zao,
siku za kale.
2 # Kut 15:17; Kum 7:1; Yos 10:42; 3:10; Mdo 7:45; Isa 60:21; Amu 4:23; 2Nya 14:13; Za 80:9; Yer 32:23 Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa
na ukawapanda baba zetu,
uliangamiza mataifa
na kuwastawisha baba zetu.
3 # Yos 24:12; Kut 15:16; Za 78:54; 77:15; 79:11; 89:10, 15; Isa 40:10; 52:10; 63:5; Kum 4:37 Sio kwa upanga wao waliipata nchi,
wala si mkono wao uliwapatia ushindi;
ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume,
na nuru ya uso wako,
kwa kuwa uliwapenda.
4 # Za 24:7; 5:2; 21:5; 74:12 Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu,
unayeamuru ushindi kwa Yakobo.
5 # Yos 23:5; Za 60:12; 108:13; Dan 8:10 Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu;
kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.
6 # Za 33:16; Hos 1:7; Mwa 48:22 Siutumaini upinde wangu,
upanga wangu hauniletei ushindi;
7 # Kum 20:4; Ay 8:2 bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu,
unawaaibisha watesi wetu.
8 # 1Kor 1:3; Rum 2:17; Za 34:2; 52:1; 30:12; 2Kor 10:17 Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa,
nasi tutalisifu jina lako milele.
9 # Kum 8:3; 31:17; Za 43:2; 107:39; 108:11; Isa 5:15; Yos 7:12 Lakini sasa umetukataa na kutudhili,
wala huendi tena na jeshi letu.
10 # Law 26:17; Amu 2:14; Kum 28:25 Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui,
nao watesi wetu wametuteka nyara.
11 # Yer 12:3; 32:37; Law 26:33; Zek 2:6; Kum 4:27; Eze 6:8; Lk 21:24; Za 9:11; 60:1; 2Fal 17:6 Umetuacha tutafunwe kama kondoo
na umetutawanya katika mataifa.
12 # Kum 32:30; Isa 50:1; 52:3; Yer 15:13 Umewauza watu wako kwa fedha kidogo,
wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.
13 # 2Nya 29:8; Isa 30:3; Yer 25:9; 42:18; 44:8; Kum 28:37; Mik 2:6; Za 79:4; 80:6; 89:41; Eze 23:32 Umetufanya lawama kwa jirani zetu,
dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka.
14 # 1Fal 9:7; 2Fal 19:21 Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa,
mataifa hutikisa vichwa vyao.
15 # Mwa 30:23; 2Nya 32:21; Za 35:26; 34:5 Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa,
na uso wangu umejaa aibu tele,
16 # Za 42:10; 10:13; 55:3; 74:10; 1Sam 18:25; Yer 11:19; Rum 12:19 kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana,
kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.
17 # Kum 6:12; 32:18; Mit 3:1; Dan 9:13; Za 119:16, 61, 153, 176 Hayo yote yametutokea,
ingawa tulikuwa hatujakusahau
wala hatujaenda kinyume na agano lako.
18 # Za 119:51, 157 Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma;
nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako.
19 # 2Nya 14:13; Za 51:8; Isa 43:12; Ay 30:29; 3:5 Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha,
na ukatufunika kwa giza nene.
20 # Kum 32:18; Amu 4:7; Isa 43:12; Kut 20:3; Yer 5:12 Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu
au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni,
21 # 1Sam 16:7; 1Fal 8:39; Yn 2:25; Mit 15:11; Yer 12:3; 17:10; Ay 31:14; Za 139:1; Mhu 12:14; Mdo 1:24; Ufu 2:23; Rum 2:16; Ebr 4:12 je, Mungu hangaligundua hili,
kwa kuwa anazijua siri za moyo?
22 # Yer 11:19; 12:3; Isa 53:7; Rum 8:36 Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;
tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.
23 # Za 7:6; 78:65; 59:5; 74:1; 77:7 Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala?
Zinduka! Usitukatae milele.
24 # Mao 5:20 Kwa nini unauficha uso wako
na kusahau taabu na mateso yetu?
25 # Za 119:25 Tumeshushwa hadi mavumbini,
miili yetu imegandamana na ardhi.
26 # Za 102:13; 26:11; 12:5; 6:4; Hes 10:25 Inuka na utusaidie,
utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014