47
Zaburi 47
Mtawala Mwenye Enzi Yote
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.
1 #
2Fal 11:12; Za 33:3 Pigeni makofi, enyi mataifa yote,
mpigieni Mungu kelele za shangwe!
2 #
Kum 7:21; Mal 1:14; Mwa 14:18; Neh 1:5; Za 2; 6; 48:2; 95:3; Mt 5:35 Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana,
Mfalme mkuu juu ya dunia yote!
3 #
Za 18:39, 47; Isa 14:6 Ametiisha mataifa chini yetu
watu wengi chini ya miguu yetu.
4 #
Za 2:8; 16:6; 78:55; 1Pet 1:4; Amo 6:8; 8:7 Alituchagulia urithi wetu,
fahari ya Yakobo, aliyempenda.
5 #
Za 68:18; Efe 4:8 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,
Bwana kwa sauti za tarumbeta.
6 #
2Sam 22:50
Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,
mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
7 #
Zek 14:9, 19; 1Nya 16:7; Kol 3:16; 1Kor 14:15 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,
mwimbieni zaburi za sifa.
8 #
1Nya 16:31; 1Fal 22:19; Za 9:4; Ufu 4:9 Mungu anatawala juu ya mataifa,
Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
9 #
Ay 25:2; Za 46:10; 97:9 Wakuu wa mataifa wanakusanyika
kama watu wa Mungu wa Abrahamu,
kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu;
yeye ametukuka sana.