48
Zaburi 48
Sayuni, Mji Wa Mungu
Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora.
1 #
2Sam 22:4; Mik 4:1; Yer 10:6; 31:23; Za 86:10; 96:4; 99:2; 135:5; 147:5; 46:4; 87:1; 18:3; 2:6; 1Nya 16:25; Kum 33:19; Isa 2:2; 11:9; 32:16; Zek 8:3; Oba 1:17; Dan 9:16 Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,
katika mji wa Mungu wetu,
mlima wake mtakatifu.
2 #
Isa 14:13; Za 2:6; 50:2; Mao 2:15; Eze 16:14; 20:6; Yos 13:17; Mt 5:35; Yer 3:19 Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana,
furaha ya dunia yote.
Kama vilele vya juu sana vya Safoni#48:2 Safoni inaweza ikawa na maana ya mlima mtakatifu au upande wa kaskazini. ni Mlima Sayuni,
mji wa Mfalme Mkuu.
3 #
Za 122:7; 18:2 Mungu yuko katika ngome zake;
amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.
4 #
2Sam 10:1-19
Wakati wafalme walipounganisha nguvu,
waliposonga mbele pamoja,
5 #
Kut 15:16
walimwona nao wakashangaa,
wakakimbia kwa hofu.
6 #
Ay 4:14; Mwa 3:16 Kutetemeka kuliwashika huko,
maumivu kama ya mwanamke
mwenye utungu wa kuzaa.
7 #
Mwa 10:4; 41:6; 1Fal 10:22; 22:48; Eze 27:26 Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi
zilizovunjwa na upepo wa mashariki.
8 #
Yer 23:6; Mik 4:1; Zek 8:13; 14:11; Isa 2:2 Kama tulivyokuwa tumesikia,
ndivyo tulivyoona
katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote,
katika mji wa Mungu wetu:
Mungu ataufanya uwe salama milele.
9 #
Za 39:3; 6:4 Ee Mungu, hekaluni mwako
tunatafakari upendo wako usiokoma.
10 #
Kut 6:3; Isa 11:12; 24:16; 42:10; 49:6; Yos 7:9; 1Sam 2:10; Za 22:27; 100:1; 65:5; 98:3; Mal 1:1 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo,
sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia,
mkono wako wa kuume umejazwa na haki.
11 #
Za 97:8
Mlima Sayuni unashangilia,
vijiji vya Yuda vinafurahi
kwa sababu ya hukumu zako.
12 #
Neh 3:1
Tembeeni katika Sayuni,
uzungukeni mji,
hesabuni minara yake;
13 #
2Sam 20:15; Isa 26:1; Mao 2:8; Hab 2:1; Za 78:6; 71:18; 109:13 yatafakarini vyema maboma yake,
angalieni ngome zake,
ili mpate kusimulia habari zake
kwa kizazi kijacho.
14 #
Za 25:5; 73:24; Mit 6:22; Isa 25:9; 49:10; 57:18; 58:11 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele;
atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.